Pata taarifa kuu
AFRIKA-UCHUMI

Maendeleo ya binadamu na uchumi barani Afrika yanakua kwa kasi ndogo: Ripoti

Ripoti mpya ya taasisi ya bilionea Mo Ibrahim, inaonesha kuwa maendeleo ya binadamu na uchumi barani Afrika yanakua kwa kasi ndogo, huku demokrasia ikidumaa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Bilionea Mo Ibrahim
Bilionea Mo Ibrahim JUSTIN TALLIS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti yake, mfuko wa Mo Ibrahim, unasema kumekuwa na maendeleo kidogo ya ukuaji wa demokrasia na utawala bora barani Afrika tangu mwaka 2012, huku tangu mwaka 2019 hali hiyo ikisalia katika kiwango kile kile.

Ripoti imeongeza kuwa kuboreshwa kwa hali ya maisha na misingi ya kiuchumi kumeendelea kudorora kutokana na ongezeko la utovu wa usalama kwenye nchi nyingine pamoja na kuminywa kwa Demokrasia.

Hata hivyo ripoti imeonesha nchi nyingi zimepiga hatua katika kuboresha huduma za Afya, elimu na huduma nyingine za kijamii, mataifa ya Mauritius, Seychelle na Tunisia yakitajwa kuwa vinara, huku Sudan Kusini, Somalia na Eritrea yakishika mkia.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.