Pata taarifa kuu

Zambia: Mkurugenzi wa IMF asema 'ana matumani' kuhusu makubaliano ya madeni

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Kristalina Georgieva amesema "ana imani" kwamba makubaliano yanaweza kufikiwa kati ya Zambia na wakopeshaji wake, ikiwa ni pamoja na China, wakati wa ziara yake nchini humo.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Kristalina Georgieva.
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Kristalina Georgieva. AP - Patrick Semansky
Matangazo ya kibiashara

Mnamo mwaka wa 2020, Zambia, mojawapo ya nchi zinazoongoza kwa uzalishaji wa shaba duniani, ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutolipa deni lake la nje linalokadiriwa kufikia dola bilioni 17.3 tangu kuzeuka kwa janga la Uviko-19.

"Nina imani kwamba wakopeshaji watafikia makubaliano" na nchi hii, Bi Georgieva amesema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Lusaka, mji mkuu wa Zambia. "Ni wazi kwangu wakati wa ziara hii kwamba Zambia inafanya inavyopaswa, kwa hivyo ninawahimiza sana wakopeshaji kusonga mbele," ameongeza.

Nchi hiyo imetoa wito kwa "mfumo wa pamoja" wa kundi la nchi 20 tajiri duniani (G20) kwa ajili ya marekebisho ya madeni ya mataifa maskini zaidi, lakini Marekani inaishutumu China, mkopeshaji mkuu wa nchi nyingi za Afrika, kwa kupunguza kasi ya mchakato huo.

Washington inashinikiza wakopeshaji "kuifutia deni Zambia, hasa China, Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen alisema siku ya Jumatatu wakati wa ziara yake mjini Lusaka kama sehemu ya ziara yake barani Afrika.

Nchi hiyo imeboresha uhusiano wake na wafadhili wa kimataifa tangu uchaguzi wa 2021 wa Rais Hakainde Hichilema, mfanyabiashara wa zamani, baada ya miaka sita ya mlipuko wa deni chini ya Edgar Lungu, ambaye alichukua mikopo mikubwa kufadhili miradi.

IMF iliidhinisha mkopo wa dola bilioni 1.3 mwaka 2022 kusaidia Zambia kurejesha utulivu wa kifedha.

siku ya Jumanne Mkurugenzi wake alisema aliridhishwa na uboreshaji wa matumizi ya rasilimali za umma, na "mwelekeo mpya wa matumizi muhimu katika elimu na afya". "Zambia inapiga hatua kubwa katika mageuzi," Bi. Georgieva alisema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.