Pata taarifa kuu
EQUATORIAL GUINEA-SIASA

Guinea Conakry: Kiongozi wa zamani wa kijeshi kufikishwa mahakamani kwa mara ya 12 leo

Kesi ya mauaji ya Septemba 28 mwaka 2009 nchini Guinea Conakry dhidi ya kiongozi wa zamani wa jeshi la mapinduzi Kepteni Musa Dadis Camara imeendelea kusikilizwa hapo jana ambapo mawakili wanaomtetea mshirika wake katika kesi hiyo Toumba Diakite waliomtuhumu kiongozi huyo kuwa alikuwepo jirani na eneo la tukio wakati wa mauaji.

Moussa Dadis Camara,Kiongozi wa zamani wa kijeshi nchini Guinea Conakry
Moussa Dadis Camara,Kiongozi wa zamani wa kijeshi nchini Guinea Conakry © wikimedia.org
Matangazo ya kibiashara

Tuhuma ambazo mawakili wa Kepteni Dadis Camara wametupilia mbali, kama anavyoeleza hapa wakili Antoine Pelelama.

“Tupo kwenye kesi ya jinai, tupo mbele ya mahakama ya jinai na tupo katika hatua ya sheria.” Ameeleza Antoine Pelelama.

Kapteni Dadis Camara ambae amefikishwa mahakama kwa mara ya 11 hapo jana, amejitetea kwamba mwenyewe aliponea chupuchupu baada ya mauaji hayo ili kuzima ukweli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.