Pata taarifa kuu
USALAMA WA WATOTO

Watoto milioni 400 duniani hufanyiwa ukatili: Ripoti

Msikilizaji ripoti zinaonesha kuwa, kila mwaka, zaidi ya watoto milioni 400 duniani hudhalilishwa kingono au kufanyiwa ukatili, kwa mujibu wa jarida la Economist Impact, matukio mengi hata hivyo hufanywa siri kutokana na unyanyapaa kwenye jamii na kuacha vitendo hivi visishughulikiwe kisheria.

Watoto milioni 400 hupitia ukatili duniani
Watoto milioni 400 hupitia ukatili duniani © UNICEF/UN0359802/Schverdfinger
Matangazo ya kibiashara

Sasa nini kifanyike kukabiliana na vitendo hivi? Collins Orono, ni afisa kutoka shirika la Mtoto News, linalotoa elimu kuhusu matumizi salama ya kidijiti, nchini Kenya.

“ Mataifa mengi unapata ya kwamba ndio sheria zipo lakini utekelezwaji haupo. ” amesema Collins Orono.

Visa vya watoto kudhalilishwa kingono au kufanyiwa ukatili vimekuwa vikiripotiwa haswa katika mataifa yanayoshuhudia mapigano na utovu wa usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.