Pata taarifa kuu
GAMBIA- USALAMA

Ecowas yashtumu jaribio la mapinduzi ya kijeshi nchini Gambia

Jumuiaya kiuchumi ya nchi za Afrika Magahribi, ECOWAS, imeisifia vikosi vya Gambia, kwa kuzuia kile kimetajwa kama jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali ya rais Adama Barrow huku pia ikilaani jaribio hilo.

Rais wa Gambia, Adama Barrow
Rais wa Gambia, Adama Barrow REUTERS/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka kwa serikali imesema wanajeshi zaidi waliohusika kupanga njama ya mapinduzi hayo dhidi ya serikali ya rais Adama Barrow, anayehudumu kwa muhula wa pili, siku ya jumanne juma hili bado wanasakwa. 

Kwa sasa hali ya utulivu imerejea katika jiji la Najul baada ya taharuki kutanda tangu siku ya jumanne. 

Rais Barrow amekuwa madarakani tangu mwaka 2016, baada ya kumshinda kiongozi wa kiimla Yahya kwenye uchaguzi, Jamme akizamika kuhamia Equatorial Guinea. 

Rais Barrow anadaiwa haliamini jeshi la taifa hilo akilazimika kutafuta huduma za wanajeshi wa Senegal kuwa walinzi wake, huku wale wa Ghana na Nigeria wakishika doria ktika viwanja vya ndege, hili likichangia umaarufu wa Barrow kufifia. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.