Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-GHANA -USALAMA

Burkina Faso imemwagiza balozi wake nchini Ghana, kurejea nyumbani

Burkina Faso, imemwagiza Balozi wake nchini Ghana, kurejea nyumbani kwa mashauriano baada ya rais wa nchi hiyo Nana Akufo-Addo kuishtumu nchi hiyo jirani, kuwakaribisha mamluki wa Wagner kutoka nchini Urusi.

Ibrahim Traoré kiongozi wa kijeshi nchini Burkina Faso
Ibrahim Traoré kiongozi wa kijeshi nchini Burkina Faso AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Rais Akufo Addo, akiwa Marekani, katika mkutano na Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, Anthony Blinken, amesema hatua hiyo ya Burkina Faso, inatishia usalama wa nchi yake.

“Leo hii mamluki wa Urusi wako katika mpaka wetu wa kaskazini ,Burkina Faso imeingia katika mpangilio na Mali katika kuwaajira vikosi vya Wagner huko.” amesema Rais Akufo Addo.

Kauli hii ya rais Addo, imekuja wakati Waziri Mkuu wa Burkina Faso Apollinaire Kyelem de Tembela akizuru Urusi kwa ajili ya mazungumzo kati ya nchi hizo mbili.

Urusi pia imetuma mamluki wake Wagner nchini Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati, kusaidia kupambana na makundi ya kijihadi

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.