Pata taarifa kuu

Nigeria: Watu watatu wauawa katika shambulizi dhidi ya ofisi ya Tume ya Uchaguzi

Polisi ya Nigeria imesema siku ya Jumatatu imewaua watu watatu wenye silaha wakati ilipokuwa ikizuia shambulio dhidi ya ofisi ya Tume ya Uchaguzi (INEC) kusini mashariki mwa Nigeria.

Ofisi kadhaa za INEC zimeshambuliwa hivi majuzi, hasa kusini-mashariki ambapo makundi yanayotaka kujitenga yameongezeka. Msemaji wa INEC Festus Okoye amethibitisha shambulio hilo katika taarifa yake siku ya Jumatatu, akisema hilo ni tukio la tatu katika jimbo la Imo ndani ya wiki mbili.
Ofisi kadhaa za INEC zimeshambuliwa hivi majuzi, hasa kusini-mashariki ambapo makundi yanayotaka kujitenga yameongezeka. Msemaji wa INEC Festus Okoye amethibitisha shambulio hilo katika taarifa yake siku ya Jumatatu, akisema hilo ni tukio la tatu katika jimbo la Imo ndani ya wiki mbili. © RFI Hausa
Matangazo ya kibiashara

Washambuliaji walijaribu kuvamia ofisi kuu ya INEC huko Owerri, mji mkuu wa jimbo la Imo, kulingana na polisi, miezi miwili kabla ya uchaguzi wa rais katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika.

"Makao makuu ya INEC huko Owerri yalishambuliwa mapema leo asubuhi na watu wenye silaha ambao waliharibu sehemu ya jengo, samani na vifaa," msemaji wa polisi katika jimbo la Imo, Michael Abattam ameliambia shirika la habari la AFP. Majibizano ya risasi yameripotiwa, "washambuliaji watatu wameuawa na wawili wamekamatwa", ameongeza Bw. Abattam.

Mwishoni mwa mwezi Februari, Wanigeria watamchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari, jenerali wa zamani wa jeshi ambaye hatawania tena baada ya mihula miwili na rekodi inayoonekana kuwa ya janga, nchi yake ikiwa katika mzozo mkubwa wa kiuchumi na ukosefu wa usalama wa jumla.

Ofisi kadhaa za INEC zimeshambuliwa hivi majuzi, hasa kusini-mashariki ambapo makundi yanayotaka kujitenga yameongezeka. Msemaji wa INEC Festus Okoye amethibitisha shambulio hilo katika taarifa yake siku ya Jumatatu, akisema hilo ni tukio la tatu katika jimbo la Imo ndani ya wiki mbili.

Hivi majuzi IEC ilionya kuhusu tishio la kuongezeka kwa ghasia wakati wa kampeni za uchaguzi, na kuongeza kuwa imerekodi angalau mashambulizi 50 tangu kuanza kwa zoezi hilo karibu miezi miwili iliyopita.

Ingawa hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo jipya, kusini-mashariki mwa Nigeria limekuwa eneo la mashambulizi mengi yanayohusishwa na kundi la wanaharakati wanaopigania uhuru wa watu wenyeji wa Biafra (IPOB).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.