Pata taarifa kuu
SIASA-HAKI

Rais wa zamani wa Comoro Sambi ahukumiwa kifungo cha maisha kwa 'uhaini mkubwa'

Rais wa zamani wa Comoro Ahmed Abdallah Sambi, 64, ambaye pia ni mpinzani mkuu wa rais wa sasa wa nchi, amehukumiwa Jumatatu kifungo cha maisha jela katika kesi ya "uhaini mkubwa" ambayo amelaani kuwa haikukatwa katika usawa.

Rais wa zamani wa Comoros, Ahmed Abdallah Mohamed Sambi.
Rais wa zamani wa Comoros, Ahmed Abdallah Mohamed Sambi. AFP / Tony Karumba
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Usalama wa taifa ni mamlaka maalum ambayo maamuzi yake hayawezi kukatiwa rufaa. Bwana Sambi "anahukumiwa kifungo cha maisha jela na udhalilishaji wa kiraia wa haki zote za kisiasa na kiraia", yaani haki yake ya kupiga kura na kustahiki, na "Mahakama inaamuru kutaifishwa kwa mali zake kwa manufaa ya hazina ya umma", jaji kiongozi wa mahakama hiyo Omar Ben Ali ametangaza katika kikao hicho.

Bw. Sambi, ndevu nyeupe na vaei la bluu, alionekana kwa muda mfupi wiki iliyopita katika siku ya kwanza ya kesi, akionekana kudhoofika baada ya kuzuiliwa kwa kipindi cha miaka minne, huku muda wa kisheria ukiwekwa kuwa miezi minane. "Muundo wa mahakama ni kinyume cha sheria, sitaki kuhukumiwa na mahakama hii", alikuwa ametangaza, kabla ya kukataa kufika kwenye kesi wakati wote atakapoitishwa kusikilizwa.

"Alisaliti misheni aliyokabidhiwa na wananchi wa Comoro," mwendesha mashtaka Ali Mohamed Djounaid alisema siku ya Alhamisi, akiomba afungwe maisha jela.

Bw. Sambi anatuhumiwa kuhusika katika kashfa inayoitwa "uraia wa kiuchumi", inayohusisha uuzaji wa pasipoti za Comoro kwa watu wasio na uraia kutoka nchi za Ghuba. Rais huyo wa zamani (2006-2011) alikuwa amepitisha sheria mwaka 2008 kuruhusu pasi kuuzwa kwa bei ya juu kwa wale wanaotaka uraia. Njia ya kujaza hazina ya Serikali kwa kutoa ardhi ya utawala ya makaribisho, hasa kwa makumi ya maelfu ya "Mabedui", kutoka nchi za Ghuba wanaochukuliwa kuwa raia wa daraja la pili katika nchi yao na walionyimwa utambulisho.

Bw. Sambi alishutumiwa kwa ubadhirifu wa mali ndani ya mfumo wa mpango huu. Uharibifu wa mali ya serikali serikali unafikia zaidi ya euro bilioni 1.8, kulingana na mwendesha mashtaka, zaidi ya Pato la Taifa la visiwa vidogo maskini katika Bahari ya Hindi.

Ahmed Abdallah Sambi, Muislamu maarufu mwenye ndevu nyeupe na muda mwingi akiwa amevalia mavazi ya kitamaduni yanayofanana na yale ya maulama wa Iran na ambayo yalimpa jina la utani la "Ayatollah", Ahmed Abdallah Sambi alisoma Saudi Arabia, Sudan na kisha katika shule ya teolojia nchini Iran.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.