Pata taarifa kuu

Comoro: Rais wa zamani Sambi ahukumiwa kwa 'uhaini mkubwa'

Rais wa zamani wa Comoro Ahmed Abdallah Sambi, 64, aliyezuiliwa kwa miaka minne kwa kesi ya ufisadi, amefikishwa siku ya Jumatatu mbele ya Mahakama ya Usalama wa taifa huko Moroni kwa kosa la "uhaini mkubwa".

Rais wa zamani wa Comoro, Ahmed Abdallah Mohamed Sambi.
Rais wa zamani wa Comoro, Ahmed Abdallah Mohamed Sambi. AFP / Juan Barreto
Matangazo ya kibiashara

Mpinzani mkuu wa Rais wa sasa Azali Assoumani, anayeonekana kuwa mgonjwa, aliketi mbele ya mahakama inayoshughulikia kesi yake katika kashfa inayoitwa "uraia wa kiuchumi", inayohusisha uuzaji wa pasipoti za Comoro kwa watu wasio na uraia kutoka nchi za Ghuba. 

Upande wa utetezi ulipinga muundo wa Mahakama, ukiona kuwa ni "kinyume cha sheria". Mkuu wake alikuwa miongoni mwa majaji waliomsikiliza katika mahakama ya mwanzo, na kwa hivyo hawezi, "kulingana na sheria, kushiriki kwa kuchukuwa uamuzi", alisema wakili wa Ubelgiji Jan Fermon.

Rais wa zamani (2006-2011) wa visiwa vidogo katika Bahari ya Hindi amepambana ili aweze kuzungumza kabla ya mijadala mikubwa. “Muundo wa mahakama ni kinyume cha sheria, sitaki kuhukumiwa na mahakama hii,” amesema.

Hatimaye Mahakama imeamua kuahirisha kusikilizwa kwa kesi hiyo hadi siku inayofuata.

Bw. Sambi amekuwa kizuizini kabla ya kesi kwa zaidi ya miaka minne huku kikomo cha kisheria kikiwa ni miezi minane. Kwa mara ya kwanza aliwekwa chini ya kifungo cha nyumbani kwa kuvuruga usalama wa taifa mnamo mwezi Mei 2018, alifungwa miezi mitatu baadaye kuhusiana na kesi hii.

Mwezi Septemba, jaji anayechunguza kesi aliainisha upya mashtaka dhidi ya rais huyo wa zamani kama "uhaini mkubwa".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.