Pata taarifa kuu
COMORO-SAMBI-SIASA-HAKI

Comoro: Rais wa zamani Sambi aendelea kuzuiliwa nyumbani kwake

Rais wa zamani wa Comoro Ahmad Abdallah Sambi anaendelea kukabiliwa na kifungo cha nyumbani kwa takriban miaka miwili bila kufunguliwa mashtaka.

Rais wa zamani wa Comoros, Ahmed Abdallah Mohamed Sambi.
Rais wa zamani wa Comoros, Ahmed Abdallah Mohamed Sambi. AFP / Juan Barreto
Matangazo ya kibiashara

Wakili wa mwanasiasa huyo, Mahamoudou Ahamada na familia yake wamesema kuwa Sambi anashikiliwa kinyume na sheria baada ya muda wa miezi minane unaoruhusiwa kumweka mtu kizuizini kumalizika tangu kitambo bila ya kufunguliwa mashtaka.

Sambi yupo katika kifungo cha nyumbani tangu Mei 2018 na alikamatwa kwa tuhuma za kusababisha vurugu, miezi mitatu baadae aliwekwa kizuizini bila kufunguliwa mashtaka kwa madai ya rushwa, kughushi na ufujaji wa mali ya umma.

Tangu miaka miwili iliyopita, ameendelea kudhoofika kiafya na familia yake imekuwa na wasiwasi juu ya kifungo chake cha muda mrefu.

Rais wa zamani Ahmad Abdallah Sambi amewekwa kizuizini nyumbani kwake katika makazi yake Kaskazini mwa mji mkuu Moroni kwa miaka miwili sasa.

"Kwa sasa, familia yake haiwezi kumuona moja kwa moja. Tunapata tu taarifa zake kutoka kupitia mtu ambaye ana ruhusa ya kwenda kumuona, " amesema binti yake Tisslame Sambi.

Ahmad Abdallah Sambi, alikuwa rais wa Comoro kuanzia mwaka 2006 hadi 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.