Pata taarifa kuu

Ajali ya basi dogo yaua takriban watu 19 nchini Misri

Takriban watu 19 wamefariki dunia Jumamosi, Novemba 12, na sita kujeruhiwa wakati basi lao dogo lilipopinduka kwenye barabara katika eneo la Nile Delta, kaskazini mwa Misri, imesema Wizara ya Afya, kulingana na shrika la habari la  AFP.

ajali hii imetokea kwenye barabara katika eneo la Nile Delta,
ajali hii imetokea kwenye barabara katika eneo la Nile Delta, Domaine public/Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Ajali za barabarani hutekea mara kwa mara nchini Misri ambapo barabara mara nyingi hazitunzwi vizuri na sheria za barabarani hazizingatiwi.

Watu 7,000 walipoteza maisha katika ajali za barabarani mnamo 2021 katika nchi yenye watu wengi zaidi katika ulimwengu wa Kiarabu, ambayo ina wakaazi milioni 104.

Mnamo mwezi Julai, watu 25 walikufa na wengine 35 kujeruhiwa wakati basi lao lilipogonga lori lililokuwa limeegeshwa kando ya barabara katikati mwa Misri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.