Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Umoja wa Mataifa: Watu milioni nane wako katika hatari ya njaa nchini Sudan Kusini

Takriban watu milioni nane nchini Sudan Kusini, theluthi mbili ya watu wote wako katika hatari ya kukabiliwa na uhaba wa chakula na njaa, Umoja wa Mataifa umeonya katika ripoti iliyotolewa Alhamisi wiki hii.

Njaa ilitangazwa nchini Sudan Kusini mwaka 2017 katika kaunti za Leer na Mayendit katika Jimbo la Unity, maeneo ambayo mara nyingi yamekuwa sehemu kubwa ya ghasia. Mwezi uliopita, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ilikadiria kuwa takriban watu 909,000 wameathiriwa na mafuriko nchini Sudan Kusini, huku mvua kubwa ikinyesha na kuharibu mazao na kuharibu makazi.
Njaa ilitangazwa nchini Sudan Kusini mwaka 2017 katika kaunti za Leer na Mayendit katika Jimbo la Unity, maeneo ambayo mara nyingi yamekuwa sehemu kubwa ya ghasia. Mwezi uliopita, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ilikadiria kuwa takriban watu 909,000 wameathiriwa na mafuriko nchini Sudan Kusini, huku mvua kubwa ikinyesha na kuharibu mazao na kuharibu makazi. © Michele Spatari, AFP
Matangazo ya kibiashara

"Njaa na utapiamlo vinaongezeka katika maeneo ya Sudan Kusini yaliyoathiriwa na mafuriko, ukame na migogoro, na baadhi ya jamii ziko katika hatari ya njaa ikiwa msaada wa kibinadamu hautadumishwa na hatua za kukabiliana na majanga hazitadumishwa, imesema ripoti hiyo.

Ripoti ya pamoja ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) inaonyesha kuwa idadi ya watu wanaokabiliwa na hali ya juu ya uhaba wa chakula na utapiamlo "haijawahi kuwa ya juu", kupita viwango vilivyoonekana hata wakati wa mzozo wa 2013 na 2016.

Kulingana na ripoti hiyo, watu milioni 7.76 wako katika hatari ya kukabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia mezi wa Aprili hadi Julai 2023, wakati watoto milioni 1.4 watakabiliwa na utapiamlo.

Ripoti hiyo inalaumu mchanganyiko wa migogoro, hali mbaya ya uchumi mkuu, hali mbaya ya hewa na kuongezeka kwa gharama za chakula na mafuta, pamoja na kushuka kwa ufadhili wa programu za kibinadamu. "Tumekuwa katika hali ya kuzuia njaa mwaka mzima na kuepusha matokeo mabaya zaidi, lakini hiyo haitoshi," Makena Walker, kaimu mkurugenzi wa WFP nchini Sudan Kusini amesema katika taarifa yake.

"Sudan Kusini iko mstari wa mbele katika mgogoro wa Tabia nchi na siku baada ya siku familia zinapoteza makazi yao, mifugo yao, mashamba yao na matumaini yao kutokana na hali mbaya ya hewa," ameongeza Bi Walker. "Bila ya msaada wa chakula cha kibinadamu, mamilioni zaidi watajikuta katika hali mbaya zaidi na kushindwa kutoa chakula cha msingi zaidi kwa familia zao."

Njaa ilitangazwa nchini Sudan Kusini mwaka 2017 katika kaunti za Leer na Mayendit katika Jimbo la Unity, maeneo ambayo mara nyingi yamekuwa sehemu kubwa ya ghasia. Mwezi uliopita, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ilikadiria kuwa takriban watu 909,000 wameathiriwa na mafuriko nchini Sudan Kusini, huku mvua kubwa ikinyesha na kuharibu mazao na kuharibu makazi.

Nchi changa zaidi duniani, Sudan Kusini imekabiliana na mizozo mikali, majanga ya asili, kuzorota kwa uchumi na mizozo ya kisiasa isiyoisha tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa Sudan mwaka 2011. Imetumia zaidi ya nusu ya maisha yake katika vita, huku takriban watu 400,000 wakiuawa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mitano vilivyomalizika mnamo 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.