Pata taarifa kuu

Mazungumzo yanaendelea kati ya waasi wa Tigray na serikali ya Ethiopia mjini Pretoria

Waasi wa jimbo la Tigray na serikali ya Ethiopia wameanza tena mazungumzo nchini Afrika Kusini siku ya Jumatano ili "kutafuta suluhu la amani na la kudumu" ya mzozo huo ambao umekumba kaskazini mwa Ethiopia kwa takriban miaka miwili.

Kabla ya mazungumzo kati ya waasi wa Tigray na wajumbe wa serikali kuu ya Ethiopia, sehemu ya jamii ya Tigray walikusanyika Pretoria, Afrika Kusini, kuandamana dhidi ya mzozo huo, Oktoba 12, 2022.
Kabla ya mazungumzo kati ya waasi wa Tigray na wajumbe wa serikali kuu ya Ethiopia, sehemu ya jamii ya Tigray walikusanyika Pretoria, Afrika Kusini, kuandamana dhidi ya mzozo huo, Oktoba 12, 2022. AP - Themba Hadebe
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya, chini ya mwamvuli wa Umoja wa Afrika (AU), yalianza Jumanne mjini Pretoria, kwa mujibu wa ofisi ya rais wa Afrika Kusini, ikibainisha kwamba yataeendelea hadi Jumapili.

Siku ya Jumatano asubuhi, washiriki kadhaa, akiwemo Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo na Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta, ambao waandishi wa habari wa shirika la habar la AFP liliwaona wakiingia katika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa ajili ya kuanza tena mazungumzo. Hakuna taarifa iliyovuja kwenye maudhui ya mazungumzo haya na vyombo vya habari vimewekwa mbali.

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, AU, Moussa Faki, Jumanne alipongeza juhudi hizi za "kunyamazisha bunduki kuelekea Ethiopia iliyoungana, tulivu, yenye amani na uthabiti".

Waasi wa Tigray na jeshi la shirikisho - wakisaidiwa na vikosi kutoka mikoa jirani ya Ethiopia na jeshi la Eritrea, nchi inayopakana na Tigray - wamekuwa wakipigana tangu mwezi Novemba 2020 katika mzozo mbaya ambao umeitumbukiza kaskazini mwa Ethiopia katika mgogoro mkubwa wa kibinadamu.

Baada ya mapatano ya miezi mitano, mapigano yalianza tena mwezi Agosti. Vikosi vya Ethiopia na Eritrea hivi majuzi vilitangaza kuwa vimeteka miji kadhaa, ikiwa ni pamoja na Shire, mojawapo ya miji mikuu ya Tigray.

Umoja wa Mataifa umeshtushwa na ghasia hizi mpya, ambazo zinazuia utoaji wa misaada kwa eneo hili lenye wakazi milioni sita. Kamishna wake Mkuu wa Wakimbizi, Filippo Grandi, Jumanne aliwataka wapiganaji, "kwa manufaa ya raia wao", kufungua "njia ya amani".

Mkuu wa diplomasia ya Marekani Antony Blinken alitoa wito kwa wahusika "kushiriki kwa umakini katika mazungumzo haya ili kufikia suluhu la kudumu la mzozo". Washington ilikuwa imeeleza kuwa mjumbe wake Mike Hammer alishiriki katika hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.