Pata taarifa kuu

Washington yatoa dola milioni 350 kwa ujenzi wa barabara nchini Malawi

Marekani siku ya Jumatano iliidhinisha ruzuku ya dola milioni 350 kwa miradi ya miundombinu nchini Malawi, ikipongeza utawala bora katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

Watu wamesimama upande wa pili wa barabara iliyoharibiwa na Dhoruba ya Tropiki Ana kando ya Barabara Kuu M1 Chikwawa nchini Malawi mnamo Januari 26, 2022.
Watu wamesimama upande wa pili wa barabara iliyoharibiwa na Dhoruba ya Tropiki Ana kando ya Barabara Kuu M1 Chikwawa nchini Malawi mnamo Januari 26, 2022. GERALD NTHALA via REUTERS - GERALD NTHALA
Matangazo ya kibiashara

Msaada huo utakaopitia shirika la Millennium Challenge Corporation, unaonuiwa kuzisaidia nchi zinazoendelea ambazo zinakidhi baadhi ya vigezo vya kidemokrasia, utatumika hasa kujenga barabara nchini ili kuunganisha maeneo ya vijijini na mijini.

Katika hafla ya utiaji saini mjini Washington, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alipongeza dhamira ya Rais Lazarus Chakwera ya "mageuzi ya kidemokrasia na kiuchumi" na kuutaja mradi wa mtandao wa barabara kuwa muhimu katika kuongeza uzalishaji wa kilimo nchini humo.

"Itakuwa ruzuku kwa Malawi - sio deni," Blinken alisema, tofauti na China, ambayo inawekeza kwa kiasi kikubwa barani Afrika katika mfumo wa mikopo ambayo Washington inaiona kuwa ni mbaya.

Bw Chakwera alishinda uchaguzi wa urais wa 2020 katika kampeni dhidi ya ufisadi katika nchi hiyo maskini ya kusini mwa Afrika.

"Serikali yangu imechagua sera ya kutovumilia kabisa rushwa, hakuna mtu anayeweza kukwepa mahakama," Rais wa Malawi amesema katika sherehe hizo.

Pia ametoa wito kwa Marekani kuunga mkono mradi wa pamoja na Zambia na Msumbiji ambao utaipatia Malawi isiyo na bahari njia endelevu ya kuingia katika Bahari ya Hindi.

Utawala wa Biden unatilia maanani umuhimu wa Afrika katika kukabiliana na ushindani kutoka kwa Urusi na hasa China, ambayo imepiga hatua kubwa katika miaka ya hivi karibuni katika bara la Afrika, kupitia uwekezaji mkubwa katika miundombinu na rasilimali za madini.

Rais Joe Biden anatarajiwa kuwapokea viongozi wa Afrika kuanzia Desemba 13 hadi 15 kwa mkutano wa kilele ambao utakuwa "ishara umuhimu wa uhusiano kati ya Marekani na Afrika".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.