Pata taarifa kuu
MALAWI-AFYA

Dozi karibu 17,000 ya chanjo aina ya AstraZeneca zaharibiwa Malawi

Malawi imeharibu dozi karibu 17,000 ya chanjo aina ya AstraZeneca ambazo ziliisha muda wa matumizi katikati ya mwezi Aprili.

Malawi imerekodi idadi kubwa ya maambukizi ya COVID-19 mwezi huu.
Malawi imerekodi idadi kubwa ya maambukizi ya COVID-19 mwezi huu. AMOS GUMULIRA AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya afya imeshtumu taarifa za uongo na propaganda ambazo zimesababisha raia wan chi hiyo kushindwa kujitokeza kwa wingi kupata chanjo hiyo.

Waziri wa afya Kumbize Kandodo amesema licha ya kuharibiwa kwa chanjo hizo serikali inahakikisha kuwa kuna chanjo za kutosha kwa ajili ya raia wa nchi hiyo. 

« Niwahakikishie raia wa Malawi kuwa wasiwe na wasiwasi baada ya kuharibu chanjo hizi, na sasa tutakabiliwa na uhaba, hapana, kama nchi  bado kuna zile ambazo tunazozitumia kwa sasa, lakini pia tutapata chanjo zaidi na lengo letu ni kuhakikisha kuwa raia wa Malawi Milioni 11 wanapata chanjo aina ya AstraZeneca ».

Tangu ilipoanza kutoa chanjo kwa raia wake, Malawi imewafikia watu 300,000 kati ya watu Milioni 11 nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.