Pata taarifa kuu
MALAWI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Wauguzi wagoma Malawi

Wauguzi nchini Malawi wamegoma kulalamikia hatua ya serikali kushindwa kuwaajiri wauguzi zaidi na kuwapa vifaa vya kujilinda wakati huu wa janga la Corona.

Mhubiri wa mitaani huko Lilongwe, Malawi. Baadhi ya raia wa nchi za Kiafrika wanajaribu kufanya ibada zao na sala kwa kukabiliana na janga la Covid-19.
Mhubiri wa mitaani huko Lilongwe, Malawi. Baadhi ya raia wa nchi za Kiafrika wanajaribu kufanya ibada zao na sala kwa kukabiliana na janga la Covid-19. AFP PHOTO / AMOS GUMULIRA
Matangazo ya kibiashara

Serikali ilikuwa imeahidi kuwaajiri maafisa 2000 wa afya ili kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Kufikia tarehe 2 Aprili, nchi 18 zilikua zimeripoti visa vya Covid-19 kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.

Mataifa kadhaa ya Afrika zimeweka mazuio ili kupambana na ueneaji wa virusi vya corona.

Afrika Kusini ilitangaza kuwa ni janga la kitaifa na kutangaza marufuku ya safari za kutoka nchi zilizoathiriwa na virusi, huku Kenya nayo ikiweka zuio kama hilo.

Hatua hizo ni jaribio la kuzuia mlipuko wa virusi katika bara hilo lenye mifumo duni ya kiafya.

Benin, Liberia, Somalia na Tanzania ni nchi zilizoripoti kuwa na wagonjwa wa kwanza wa virusi hivyo.

Tanzania ambayo inaendelea kukumbwa na janga la Covid-19, haijachukua hatua yoyote kama vile raia kupigwa marufuku kutoka nje, kuzuia mikusanyiko ya watu, ambapo sala na ibada mbalimbali zinaendelea kufanyika makanisani na misikitini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.