Pata taarifa kuu

Katiba Mpya: Mahakama ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yafuta agizo za Rais Touadera

Mahakama ya Katiba imefuta agizo zinazounda kamati inayohusika na kandika Katiba mpya, kwa ombi kutoka upinzani ambao ulihofia kuwa sheria mpya mama itampa mamlaka Mkuu wa Nchi kugombea muhula wa 3.

Mnamo Agosti 27 huko Bangui, waandamanaji waliandamana kupinga pendekezo la mabadiliko ya katiba ambayo yatamruhusu Félix Archange Touadéra kugombea muhula wa tatu.
Mnamo Agosti 27 huko Bangui, waandamanaji waliandamana kupinga pendekezo la mabadiliko ya katiba ambayo yatamruhusu Félix Archange Touadéra kugombea muhula wa tatu. AFP - BARBARA DEBOUT
Matangazo ya kibiashara

Agizo hizo "zinakiuka katiba na ni batili", umebaini uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Juu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, nchi ya pili kwa umaskini duniani, inayokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa karibu miaka tisa. "Marekebisho ya Katiba yanaweza tu kufanywa baada ya kuwekwa kwa Bunge la Seneti", ambalo halijawekwa nchini, unasisitiza uamuzi huo.

Uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika mwezi Septemba, wa kwanza katika kipindi cha miaka 34, ulifutwa kwa kukosa fedha za kuuandaa. Mameya waliochaguliwa walipaswa kuteua maseneta, na hivyo kuzuia kuanzishwa kwa Bunge la Seneti.

Mahakama ya Katiba pia inaeleza kwamba mpango wa kura ya maoni kuhusu marekebisho ya katiba ni wa Rais, lakini hilo haliwezi kufanywa kwa kukiuka kiapo kilichotolewa na Bw. Touadéra wakat alipotawazwa.

Bw. Touadéra aliapa "Naapa mbele ya Mungu na mbele ya taifa kuzingatia Katiba kwa makini (...) kutotumia mamlaka niliyopewa na Katiba kwa ajili ya maslahi yangu binafsi wala kurekebisha idadi na muda wa muhula wangu wa madaraka, "uamuzi unasema.

Mwishoni mwa mwezi wa Agosti, Bw. Touadéra, aliyechaguliwa mwaka wa 2016 na kuchaguliwa tena mwaka wa 2020 baada ya uchaguzi uliyopingwa na upinzani, aliunda kamati yenye jukumu la kuandaa rasimu ya Katiba mpya. "Sauti nyingi zaidi zinaongezeka kutaka Katiba ibadilishwe," alisema.

Kamati hii ilikuwa inaundwa na wajumbe 53 "wakiwakilisha mikondo yote ya maoni", wakiwemo wawakilishi wa Bunge, vyama vya siasa vya walio wengi, upinzani na mashirika ya kiraia, linabaini agizo hilo lililobatilishwa. Kwa miezi kadhaa, mamlaka imepanga maandamano ya kuunga mkono marekebisho ya Katiba.

"Huu ni ushindi wa kishindo kwa wanademokrasia wote, popote walipo," amesema Bw. Crépin Mboli-Goumba, mmoja wa waliokata rufaa, siku ya Ijumaa, na kuongeza: "Ningependa kutoa pongezi zinazostahili kwa Mahakama ya Katiba ya nchi yetu. ", haswa kwa rais wa taasisi hii ambaye "ameokoa demokrasia", alitangaza.

MINUSCA yaimarisha ulinzi

Siku ya Ijumaa asubuhi, kikosi kikubwa cha askari, maafisa wa polisi na wajumbe wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) waliwekwa kando ya barabara inayoelekea Mahakama ya Ktiba na ni waandishi wa habari na wanasheria pekee ndio waliweza kuingia kwenye mahakama hiyo, amebainisha mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP.

Walinda amani 14,000 wa Umoja wa Mataifa ambao sasa kimsingi wana jukumu la kulinda raia - wamekuwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu mwezi wa Aprili 2014. Kutumwa kwao kulilenga kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya umwagaji damu vilivyoanza mwaka 2013 baada ya mapinduzi dhidi ya rais François Bozize.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.