Pata taarifa kuu
CAR-MAZUNGUMZO

Mazungumzo ya amani CAR yakwenda kombo

Mazungumzo ya amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo yamekuwa yakiendelea, yamemalizika bila ya kuwepo kwa makubaliano yoyote.

Mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui.
Mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui. DR
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yalimalizika mwishoni mwa wiki iliyopita, bila ya ushiriki wa makundi ya waasi na wanasiasa wa upinzani ambao waliususia.

Kulikuwa na mvutano  wakati wa mazungumzo hayo, baada ya pendekezo kuwa raia awanie kwa muhuma wa tatu, pendekezo ambalo baadaye liliondolewa, na wakati wa kutamatisha mazugumzo hayo, mapendekezo 600 yaliwasilishwa, na mojawapo ya mapendekezo ilikuw ani kuondoa marufu ya uingizwaji wa silaha nchini humo, hatua iliyowekwa na umoja wa Mataifa mwaka 2013 baada ya makundi ya waasi kumwondoa madarakani rais Francois Bozize.

Mazungumzo hayo yalianza Machi 21, kati ya serikali, wanasiasa wa upinzani na viongozi wa serikali za mitaa, baada ya rais Faustin-Archange Touadéra mwaka 2020 kuahidi kuwa serikali yake itaanda mazungumzo yanayolenga kuleta maridhiano nchini humo.

Watalaam wa siasa za Jamhuri ya Afrika ya Kati, wanaona kuwa ajenda ya mazungumzo hayoa, haikuwa na uzito na serikali imekuwa ikilenga kuifurahisha Jumuiya ya Kimataifa.

.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.