Pata taarifa kuu

Jamhuri ya Afrika ya Kati: Mahakama ya Katiba yakumbwa na mvutano mkubwa

Mahakama ya Kikatiba inatazamiwa kutoa uamuzi uliokuwa ukingojewa hadi mwisho wa mwezi. Ni lazima iamue ombi lililowasilishwa na jukwaa la upinzani la BRDC (Kambi ya Jamhuri ya Kutetea Katiba) dhidi ya agizo la rais la kuunda tume ya kuandaa Katiba mpya ya nchi. Wajumbe wake wanalengwa na maandamano na vitisho, ambavyo vinaweka shinikizo kwa taasisi hiyo, kulingana na upinzani.

Danièle Darlan, Jaji mkuu wa Mahakama ya Kikatiba ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Danièle Darlan, Jaji mkuu wa Mahakama ya Kikatiba ya Jamhuri ya Afrika ya Kati. © Gaël Grilhot/RFI
Matangazo ya kibiashara

Je, majaji wanane wa Mahakama ya Kikatiba wataweza kutoa uamuzi wao kwa utulivu kamili?

Upinzani kwa ambao wametoa ombi hilo hauogopi: unalaani mashambulizi, na hata vitisho, kutoka kwa makundi yenye misimamo mikali dhidi ya taasisi hiyo, ili kuilazimisha kuhalalisha mchakato wa mabadiliko ya Katiba.

Kulingana na BRDC, saauti zimepazwa tangu Mahakama ilikataa baadhi ya masharti ya mradi wa huo mwishoni mwa mwezi wa Agosti.

Alhamisi na Ijumaa, waandamanaji mia kadhaa, wakiwa na mabango yaliyoandikwa maneno ya kuchochea uhasama, walikusanyika mbele ya makao makuu yao, yaliyowekwa chini ya ulinzi wa vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA), kutaka hasa kuondoka kwa Danièle Darlan, ambaye amekuwa mwenyekiti wa taasisi hiyo tangu mwaka wa 2017.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, kongamano la wabunge wanawake wa Jamhuri ya Afrika ya Kati lilisema kuwa lilikashifiwa.

Chama cha Wanasheria kilitaka mkutano mkuu wa taaluma mbalimbali za sheria siku ya Jumatano asubuhi, kukemea "matishio ya mara kwa mara dhidi ya taasisi za mahakama"

Waziri wa Usalama wa Umma kwa upande wake alipiga marufuku maandamano mbele ya Mahakama. Shirika lililo karibu na mamlaka na linalopendelea mageuzi, Republican Front linataka "kuwaacha majaji kuwa na uhuru wao kamili".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.