Pata taarifa kuu
DRC- SIASA

DR Congo: Mawakili wa Francois Beya wamejiondoa.

Mawakili wa aliyekuwa mshauri wa masuala ya usalama wa taifa kwa rais Felix Tschisekedi, wametangaza kujiondoa kumuwakilisha mteja wao kwa kile wanasema mahakama inayosikiliza kesi hiyo kuwa na upendeleo.

François Beya,aliyekuwa mshauri wa masuala ya usalama wa kitaifa kwa rais wa DR Congo Félix Tshisekedi
François Beya,aliyekuwa mshauri wa masuala ya usalama wa kitaifa kwa rais wa DR Congo Félix Tshisekedi © Service de communication de la Haute Cour
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yao, mawakili hao wameandika barua kwa mahakama ya kijeshi inayosikiliza kesi dhidi ya Francois Beya, wakitaka majaji walioko kubadilishwa na kutangazwa wapya ambao watakuwa hawana upendeleo.

Beya aliyefahamika sana kama Mr Security kutokana nakuwa karibu na Tschisekedi, anashtakiwa na watu wengine 6, wakiwemo wanajeshi na polisi, ambao kwa pamoja wanatuhumiwa kwa makossa ya uhaini, ikiwemo kupanga njama za kumdhuru rais.

Wakili kiongozi wa jopo la utetezi, John Kaboto, amesema wamefikia uamuzi wa kujitoa kwenye kesi hiyo, kutokana na ushahidi kuchezewa pamoja na upendeleo wa wazi ulioneshwa na majaji katika kesi hiyo, wakili Kaboto akimuombea mteja wake dhamana ili akapatiwe matibabu.

Beya amehudumu kwa nyakati tofauti na viongozi mbalimbali waliotawala taifa hilo, akiwemo Mobutu Sese Seko, ambapo alipewa jina la Fantomas, likimaanisha mtu asiyeonekana licha ya majukumu aliyonayo.

Beya na wenzake walikamatwa Februari 5 mwaka huu pamoja na viongozi wengine wajuu katika jeshi la Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.