Pata taarifa kuu
AFRIKA MASHARIKI- MAZINGIRA.

Rais Samia anawataka maaskofu kuhubiri injili ya utunzaji mazingira.

Rais wa Jamuhuri ya Tanzania, Samia Suluhu, ametoa wito kwa viongozi wa dini kutangaza injili ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa wafuasi wao.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan © blog.ikulu.go.tz
Matangazo ya kibiashara

Rais Samia ameeleza ujumbe wa utunzi wa mazingira ni muhimu sana haswa wakati huu ambapo dunia inapokabiliwa na athari zinazotokana na uharibifu wa misitu, athari ambazo pia zimeathiri binadamu.

Rais Samia ametoa wito huu wakati wa sherehe za shirikisho la maaskofu wa kanisa katoliki Afrika Mashariki (AMECEA).

Kwa mujibu wa rais Samia, baadhi ya maeneo yamekuwa yakishuhudia viwango vya juu vya joto na mafuriko hali ambayo haikuwepo awali akitaja changamoto hii kuwa imechangiwa na shughuli za bindamu katika uharibifu wa mazingira.

Kama njia moja ya kutilia mkazo wito wake, rais alinuku kifungu cha bibilia kinachosisitiza kuhusu ulindaji wa mali asilia ambao ilipeanwa na Mungu.

AMECEA ni mkutano amabo umeandaliwa na viongozi wa kanisa katoliki kutoka nchini Eritrea, Ethiopia, Malawi, Kenya, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania, Uganda, na Zambia.

Kauli mbiu ya mkutano huo wa maaskofu mwaka huu ni kujadili kuhusu umuhimu wa mazingira pamoja na kuwahamasisha wafuasi wao kuhusu utunzi wa mazingira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.