Pata taarifa kuu

Jean-Claude Gakosso: Libya "lazima ipitie kwenye maridhiano"

Kufuatia kazi yake ya siku kadhaa nchini Libya, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo, Jean-Claude Gakosso, ambaye nchi yake ni mwenyekiti wa Kamati ya Ngazi ya Juu ya majadiliano juu ya Libya, anaunga mkono hitaji la kuandaa mkutano wa maridhiano ya kitaifa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo Jean-Claude Gakosso wakati wa kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Jumamosi, Septemba 28, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo Jean-Claude Gakosso wakati wa kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Jumamosi, Septemba 28, 2019. AP - Jeenah Moon
Matangazo ya kibiashara

Mbele ya serikali mbili hasimu zinazogombania madaraka na uhalali, nchi imegawanyika zaidi kuliko wakati mwingine wowote na "lazima kabisa kupitia maridhiano" anasema Jean-Claude Gakosso ambaye aliongoza ujumbe wa Afrika uliozuru Tripoli. Hatua muhimu, hasa baada ya kushindwa kufanyika kwa uchaguzi na mwisho wa kipindi cha kuafikiwa kwa makubaliano yaliyopatikana chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kusitisha mapigano.

"Jumuiya ya kimataifa bado inahitaji kufanya juhudi za kuwarejesha Walibya kwenye meza ya mazungumzo ili kuondokana katika ombwe la aina hii la kisiasa kwani uchaguzi haukuweza kufanyika mwaka jana," ameongeza awakati alipokuwa akihojiwa na Houda Ibrahim, kutoka kitengo cha RFI katika kanda ya Afrika.

"Kwa upande wake, Umoja wa Afrika na Kamati yake ya Ngazi ya Juu, inayoongozwa na Rais [Denis] Sassou-Nguesso, wanafanya kinachowezekana kwa ajili ya kufanyika kwa mkutano wa maridhiano, kwa sababu tunaona kuwa uchaguzi huo sio dawa ya matatizo ya Libya." , amebaini Jean-Claude Gakosso.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.