Pata taarifa kuu
DRC

Aliyekuwa mshauri wa masuala ya usalama wa rais Thisekedi kufikishwa Mahakamani

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, aliyekuwa mshauri wa rais Felix Tshisekedi kuhusu masuala ya usalama François Beya, atafikishwa katika Mahakama ya kijeshi siku ya Ijumaa.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo  Félix Tshisekedi
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi © Arsène Mpiana / AFP
Matangazo ya kibiashara

Beya na mwenzake watano wanakabiliwa na mashataka ya kupanga njama ya kumshambulia rais wa Jamhuri, kati ya mwaka 2020 hadi mapema mwezi Februari mwaka 2022.

Aidha, amedaiwa kuwa bila ya kuwa na idhini kutoka Wizara ya Ulinzi na Ofisi ya rais, aliagiza ununuzi wa silaha za kijeshi kutoka kwa kampuni moja kutoka nchini Ubelgiji.

Mwaka 2021, Beya anaripotiwa kusafiri kwenda jijni Harare nchini Zimbabwe, kukutana na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Jenerali John Numbi, anayedaiwa kuhusika na mauaji ya wanaharakati Floribert Chebeya na  Fidel Bazana.

Mahakama ya kijeshi inamshutumu kwa kutompa tarifa rais Tshisekedi kuhusu kuwepo kwa mpango wa kuwepo kwa mipango ya uhaini.

Katika hatua nyingine, rais Tshisekedi amewaachisha kazi wanajeshi wanne wenye nyadhgifa za juu katika jeshi la nchi hiyo baada ya uamuzi wa Baraza kuu la usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.