Pata taarifa kuu

Mkutano wa AU: Dola milioni 140 zakusanywa kukabiliana na majanga ya kibinadamu

Siku ya maafa ya kibinadamu ilimalizika Ijumaa jioni huko Malabo, Equatorial Guinea.

Nchini CAR, kunaripotiwa mzozo wa kiusalama na wa kibinadamu. Hapa, Waislamu waliokimbia makazi yao huko PK5.
Nchini CAR, kunaripotiwa mzozo wa kiusalama na wa kibinadamu. Hapa, Waislamu waliokimbia makazi yao huko PK5. REUTERS/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

Siku nzima, hotuba za Wakuu wa Nchi zilizingatia sababu za changamoto nyingi zinazokabili bara la Afrika. Miongoni mwa changamoto hizo ni migogoro ya kibinadamu ambayo chanzo chake ni migogoro ya kivita. Ikiongezwa hii leo na ugaidi, itikadi kali, mabadiliko ya tabia nchi na kusababisha mafuriko na ukame. Mambo ambayo mara nyingi husababisha watu kuhama.

Ili kukabiliana na changamoto hizi, serikali na wafadhili wamerejesha dhamira yao kwa lengo hilo kwa kuchangisha fedha. Uhamasishaji wa washirika umewezesha kupata dola milioni 140 kutoka kwa hitaji la dola bilioni 14 kutunza watu waliohamishwa na wakimbizi.

Umoja wa Afrika umesema katika taarifa  nchi 15 ambazo zimeathiriwa mno zinahitaji misaada ya haraka hasa wakati huu ambao athari za mabadiliko ya tabia nchi zinafanya mahitaji ya kibinadamu kuongezeka kwa kiwango kikubwa. Umoja huo umetilia maanani kuwa miongoni mwa watu milioni 30 waliopoteza makaazi yao, zaidi ya milioni 10 ni Watoto wenye umri wa chini ya miaka 15. Hali hiyo inasababishwa na mizozo ya kikabila na tatizo la upatikanaji wa chakula usiokuwa wa uhakika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.