Pata taarifa kuu

DRC: Rais Tshisekedi kushugulikia mapungufu kwenye vyombo vya usalama.

Rais wa DRC Félix Tshisekedi ameahidi kukomesha mazoea yote mabaya yanayosababisha vyombo vya usalama vinashindwa kuimarisha Usalama-nchini mwake na kawataka wanajeshi wa nchi hiyo  kuzingatia nidhamu ndani ya Jeshi na Vyombo hivyo.

Rais wa DRC Félix Tshisekedi.
Rais wa DRC Félix Tshisekedi. © Arsène Mpiana / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii ameitoa rais Felix Tshisekedi wa DRC wakati wa  kuifungua semina inayozingatia nidhamu na maadili ya kijeshi katika Shule inayotoa mafunzo ya Kijeshi huko Kinshasa, amhamis ya wiki Hii.

Katika taarifa ya ikulu ya rais, ni kwamba Tshisekedi aliitumia fursa hiyo kushutumu hadharani tabia potovu ya baadhi ya wanjeshi ambao alisema wanajihusisha na vitendo vilivyo kinyume na maadili na mafundisho ya kijeshi, huku akisema kuwa Ni wakati wa kukomesha vitendo vyote vya mauaji raia wasio na hatia, katika Nchi yake.

Huu sio muda wa kuzingatia wazo la kushirikisha  pamoja jeshi la FARDC na vikundi vyenye silaha kupigana na kundi lingine lenye silaha, akitoa mfano wa mapambano dhidi ya kundi la M23.

Matamshi akiyatoa siku nne tu zimepita ambapo makundi manne yenye silaha yaliahidi kusitisha uhasama kati yao na kuunga mkono FARDC dhidi ya tishio lolote la nje.

Mkataba wa kutoshambuliana kati ya wanamgambo hao ulitiwa saini katika mkutano uliofanyika Mjini Pinga mkowani Kivu Kaskazini Mashariki mwa Nchi hiyo, ambapo walihudhuria, Janvier Karahiri wa (APCLS), Guidon Mwissa wa Nduma Defence of Congo (NDC-Rénové),Miongoni mwa wengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.