Pata taarifa kuu

Raia 14 wameuawa katika kambi ya wakimbizi jimboni Ituri nchini DRC.

Watu kumi na wanne wakiwemo watoto, wameuawa katika shambulio la hivi punde ambalo limetekelezwa katika kambi ya wakimbizi iliyoko katika eneo la Ituri mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

 Wanajeshi wa FARDC nchini DRC
Wanajeshi wa FARDC nchini DRC AFP - SEBASTIEN KITSA MUSAYI
Matangazo ya kibiashara

Mashirika ya kutetea haki za bindamu kwenye eneo hilo yameeleza kuwa shambulio hilo la siku ya jumatatu lilitokea katika eneo la Djugu huko Ituri, limeripoti shirika la Kivu Security Tracker (KST)

Waasi wa kundi la wapiganaji wa CODECO wameripotiwa kutekeleza shambulio hilo, kundi ambalo linaendeleza shughuli zake mashariki mwa kongo.

Majimbo ya Ituri na Kivu kaskazini yamekuw chini ya utawala wa kijeshi tangu mei mwaka jana kama njia moja ya kujaribu kumaliza mashambulio yanayotekelezwa na magenge ya waasi.

Licha ya uwepo wa wanalinda usalama katika maeneo husika, mashambulio ya waasi yameendelea kuripotiwa, mauaji ya raia, wanawake kwa watoto yakiripotiwa kuongezeka.

Raia wa maeneo hayo wamekuwa kwa mara kadhaa wakiwatuhumu wanajeshi wa FARDC na polisi mashariki mwa kongo kwa uzembe katika opereseheni dhidi ya makundi ya waasi.

Kundi la waasi wa CODECO na lile la (ADF),ambalo Marekani imelihusisha na kikundi cha Islamic State yakitajwa kuwa mstari wa mbele kwa mauaji ya raia.

Shambulio la hili ya siku ya jumatatu limekuja baada ya raia wengine 35 kuuwawa na waasi wakiwa katika mgodi wa kuchimba dhahabu katika eneo la Ituri ambapo waasi wa CODECO wamehusishwa.

Shinikizo imezidi kuelekezwa kwa rais Felix Tshisekedi,kutafuta mbinu ya kumaliza utovu wa usalama katika maeneo ya mashariki mwa kongo, mashambulizi yakiripotiwa kuendelea licha ya uwepo wa wanajeshi wa Uganda UPDF kusaidia katika harakati za upatikanaji wa amani. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.