Pata taarifa kuu

Afrika Kusini yatathmini uharibifu mkubwa baada ya mafuriko

Uharibifu mkubwa kutokana na mafuriko yaliyoikumba Afrika Kusini, na kuua takriban watu 443, ulikuwa unatathminiwa siku ya Jumanne, huku hali ya maafa ya kitaifa ikitangazwa wiki moja baada ya hali mbaya ya hewa kuanza katika pwani ya mashariki.

Wafanyakazi wa kujitolea wanaokota uchafu kwenye Ufukwe wa Kaskazini baada ya mvua kubwa kunyesha kwa siku chache zilizopita, huko Durban, Afrika Kusini, Aprili 15, 2022.
Wafanyakazi wa kujitolea wanaokota uchafu kwenye Ufukwe wa Kaskazini baada ya mvua kubwa kunyesha kwa siku chache zilizopita, huko Durban, Afrika Kusini, Aprili 15, 2022. © AFP, Rajesh Jantilal
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wengi walitarajiwa wakati wa mchana huko Durban, kitovu cha maafa, kukagua shule, hospitali na miundombinu iliyoharibiwa vibaya. Siku moja kabla, Rais Cyril Ramaphosa alizungumza kuhusu "janga la kibinadamu ambalo linahitaji uingiliaji kati mkubwa na wa haraka" na akatangaza hali ya maafa ya kitaifa ambayo inapaswa kuwezeshackutolewa kwa rasilimali za kipekee.

Bandari ya Durban, mojawapo ya vituo vikuu vya baharini barani Afrika na nguzo kuu ya shughuli za kiuchumi nchini humo, iliathirika pakubwa.

Mafuriko yalivamia sehemu za kusini mashariki kwa mji pwani wa Durgan mapema wiki iliyopita na kuharibu barabara, hospitali na kusomba majengo na wote waliokuwemo ndani.

Hadi sasa mafuriko hayo yameharibu nyumba 13,500, kiasi hospitali na kliniki 58 pamoja na mifumo mingine ya mawasiliano, usambazaji wa maji, nishati na barabara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.