Pata taarifa kuu

Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko nchini Afrika Kusini yaongezeka hadi watu 400

Mafuriko makubwa nchini Afrika Kusini yamegharimu maisha ya watu 400 na kuathiri karibu watu 41,000, baada ya idadi zaidi vifo kuripotiwa siku ya Ijumaa.

Watu wanatembea kwenye daraja la lilijegnwa kwa muda huko Ntuzuma, karibu na Durban, Afrika Kusini, Aprili 12, 2022.
Watu wanatembea kwenye daraja la lilijegnwa kwa muda huko Ntuzuma, karibu na Durban, Afrika Kusini, Aprili 12, 2022. AP - STR
Matangazo ya kibiashara

“Jumla ya watu 40,723 wameathirika. Kwa bahati mbaya, idadi ya waliofariki inaendelea kuongezeka, huku idadi ya vifo iliyorekodiwa hivi punde ni watu 395 ambao wamefariki dunia," ilisema Idara ya Ushirikiano na Masuala ya Jadi ya jimbo la Kwazulu-Natal mashariki mwa nchi, ambapo hali ya hatari imetangazwa.

Wengi wa waathiriwa walirekodiwa katika eneo la Durban, bandari kuu ya Afrika katika jimbo la Kwazulu-Natal na kitovu cha hali mbaya ya hewa iliyoanza wikendi iliyopita.

Mvua hizo zilizofikia viwango ambavyo havikuonekana kwa zaidi ya miaka 60, zilisomba madaraja, barabara na kutenga sehemu kubwa ya ukanda huo unaopakana na Bahari ya Hindi. Zaidi ya shule 250 zimeathirika na maelfu ya nyumba kuharibiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.