Mafuriko yaua watu 300 Afrika kusini
Watu zaidi ya 300 wamepoteza maisha katika jimbo la la KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini kufuatia mafuriko ambayo pia yamesababisha uharibifu mkubwa wa miundo mbinu katika eneo hilo.
Imechapishwa:
Hii imeelezwa kuwa dhoruba mbaya zaidi kuwahi kutokea katika taifa hilo la Afrika Kusini baada ya serikali kutangaza takwimu hizo.
Mafuriko hayo yamesababishwa na mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha katika jimbo la KwaZulu-Natal, huku maporomoko ya udongo yakishuhidiwa pia na kuwanasa watu chini ya majengo.
Watalaam wa hali hali ya hewa wanaonya kuwa mafuriko zaidi yanatarijiwa kushuhudiwa katika siku zijazo, wakati huu shughuli za kuwaokoa watu zikitatizwa na ukungu.
Mafuriko hayo makubwa yalisabisha pia kusombwa kwa mama 12 kutoka kwenye hifadhi ya wanyamapori ya Ezemvelo KZN, lakini wamepâtikana hivi leo.