Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Vita vya mfululizo katika ufalme wa Wazulu vyafikia kikomo

Ni mwisho wa mwaka wa mashaka kwa Wazulu. Baada ya kifo cha Mfalme Wema Zwelithin mnamo mwezi wa Machi 2021, mwanamfalme Misuzulu anatarajia kutawazwa kuchukuwa wadhifa kama mfalme.

Mfalme mpya wa Wazulu, Prince Misuzulu Zulu (wa pili kutoka kulia) wakati wa sherehe za kutawazwa kwenye Ikulu ya Khangelakamankegane, Mei 7, 2021
Mfalme mpya wa Wazulu, Prince Misuzulu Zulu (wa pili kutoka kulia) wakati wa sherehe za kutawazwa kwenye Ikulu ya Khangelakamankegane, Mei 7, 2021 © AFP
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya familia walipinga mahakamani juu ya kutawazwa kwake kwenye kiti kilichotangazwa na malkia. Taratibu sasa zimemailika, na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ametoa baraka zake.

Mwanamfalme Misuzulu, 47, ataweza kutawala zaidi ya Wazulu milioni 11. Kutambuliwa na Rais Ramaphosa kunakuja wiki mbili baada ya ushindi mahakamani. Mahakama ya Pietermaritzburg ilikuwa imekataa maombi ya sehemu ya familia iliyotaka kusitisha kutawazwa.

Cyril Ramaphosa hakuchukulia uamuzi huu kirahisi. Alishauriana na Waziri wake wa Masuala ya Kijadi na Waziri Mkuu wa Mkoa wa KwaZulu-Natal. Kwa sababu ikiwa mfalme wa Kizulu hana mamlaka ya utendaji, ana ushawishi wa kisiasa katika jimbo la pili kwa ukubwa la Afrika Kusini.

Mwanamfalme Misuzulu alikuwa anaungwa mkono na Chama cha Zulu Inkhata (IFP), ambacho kinakumbusha kwamba "ufalme unaunganisha taifa la Wazulu, hutoa utulivu na kulinda urithi wa ufalme". Urithi ni ardhi hasa, 30% ya mkoa inasimamiwa na jamii ya kifalme ambayo hutoza ushuru. Hii itakuwa moja ya majukumu ya mtawala wa baadaye baada ya kutawazwa kwake, ambapo tarehe yake bado haijatangazwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.