Pata taarifa kuu

Tunisia: Meli ya wafanyabiashara iliyobeba tani 750 za dizeli yazama katika pwani ya Gabes

Nchini Tunisia, meli ya mizigo imezama asubuhi ya Jumamosi hii, Aprili 16, katika Pwani ya mji wa Gabès katikati mwa nchi. Mamlaka sasa inahofia kumwagika kwa mafuta.

Meli ya mizigo iliyokuwa na tani 750 za mafuta ilizama katika Ghuba ya Gabès, kusini-mashariki mwa Tunisia.
Meli ya mizigo iliyokuwa na tani 750 za mafuta ilizama katika Ghuba ya Gabès, kusini-mashariki mwa Tunisia. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Meli hiyo  inayojulikana kwa jina la Xelo iliyokuwa na bendera ya Equatorial Guinea, iliyopitia Misri na kuelekea Malta, ilikuwa na matatizo tangu Ijumaa jioni katika Bahari ya Mediterania.

Kutokana na hali ngumu ya hewa, meli hiyo ya mizigo ilikuwa imepata kibali cha kukaribia pwani ya Tunisia. Ilipokuwa kilomita 7 kutoka Ghuba ya Gabès, kusini-mashariki mwa nchi, ilianza kuzama. Maji yaliingia kwenye chumba cha injini chenye urefu wa karibu mita mbili, kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Mazingira ya Tunisia. Dharura ilikuwa kwanza kuokoa wafanyakazi.

Si chini ya tani 750 za dizeli sasa zinahofia kumwagika kwenye maji ya Tunisia. Kutokana na uwezekano wa kumwagika kwa mafuta, Wizara ya Mazingira ya Tunisia inatangaza kwamba inafanya kila linalowezekana kudhibiti hali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.