Pata taarifa kuu
TUNISIA-USALAMA

Tunisia: Watu mia kadhaa wajeruhiwa katika ajali ya treni mbili zilizogongana

Takriban watu 100 wamejeruhiwa siku ya Jumatatu, wengi wao wakiwa wamepata majeraha madogo, katika ajali ya treni mbili ziliozogongana kusini mwa mji mkuu wa Tunis, kikosi cha Ulinzi wa Raia kimesema.

"Ajali hii ya treni mbili kugongana imesababisha watu 95 kujeruhiwa, ambao wamesafirishwa hadi hospitali," msemaji wa kikosi cha Ulinzi wa Raia, Moez Treaa ameliambia shirika la habari la AFP, na kuongeza kuwa treni moja ilikuwa imebeba abiria, huku ya pili ikiwa tupu.
Kulingana na msemaji huyo, wengi wa waliojeruhiwa walivunjika mifupa au wamepata majeraha madogo au walikuwa katika hali ya mshtuko, lakini hakuna kesi vifo iliyoripotiwa. Magari 15 ya kubebea wagonjwa na magari mengine ya dharura yametumwa kwenye eneo la ajali.
Ajali ya treni mbili za shirika la reli la Tunisia (SNCFT) imetokea mwendo wa 09:30 saa za Tunisia huko Jbel Jelloud, katika moja ya viunga vya kusini mwa mji mkuu. Sababu za ajali hiyo hazijajulikana.
Mwandishi wa shirika la habari la AFP aliyeshuhudia ajali hiyo anasema aliona sehemu ya mbele ya anakokaa dereva katika moja ya treni ikiwa imeharibika kiasi. Ajali hiyoilitokea dakika chache kabla ya kuwasili kwa treni mbili za abiria zilizokuwa zinaelekea kituo kikuu cha Tunis.
Mnamo mwezi Desemba 2016, watu watano walifariki dunia na zaidi ya 50 kujeruhiwa katika eneo moja katika ajali ya kugongana kwa basi la usafiri wa umma na treni, kutokana na ubovu wa miundombinu.
Mnamo mwezi Juni 2015, Tunisia ilikumbana na moja ya tukio mbaya zaidi katika historia yake ya hivi majuzi, na vifo vya watu 18 katika ajali kati ya treni na lori huko El Fahes, karibu kilomita sitini kusini mwa Tunis.
"Ajali hii ya treni mbili kugongana imesababisha watu 95 kujeruhiwa, ambao wamesafirishwa hadi hospitali," msemaji wa kikosi cha Ulinzi wa Raia, Moez Treaa ameliambia shirika la habari la AFP, na kuongeza kuwa treni moja ilikuwa imebeba abiria, huku ya pili ikiwa tupu. Kulingana na msemaji huyo, wengi wa waliojeruhiwa walivunjika mifupa au wamepata majeraha madogo au walikuwa katika hali ya mshtuko, lakini hakuna kesi vifo iliyoripotiwa. Magari 15 ya kubebea wagonjwa na magari mengine ya dharura yametumwa kwenye eneo la ajali. Ajali ya treni mbili za shirika la reli la Tunisia (SNCFT) imetokea mwendo wa 09:30 saa za Tunisia huko Jbel Jelloud, katika moja ya viunga vya kusini mwa mji mkuu. Sababu za ajali hiyo hazijajulikana. Mwandishi wa shirika la habari la AFP aliyeshuhudia ajali hiyo anasema aliona sehemu ya mbele ya anakokaa dereva katika moja ya treni ikiwa imeharibika kiasi. Ajali hiyoilitokea dakika chache kabla ya kuwasili kwa treni mbili za abiria zilizokuwa zinaelekea kituo kikuu cha Tunis. Mnamo mwezi Desemba 2016, watu watano walifariki dunia na zaidi ya 50 kujeruhiwa katika eneo moja katika ajali ya kugongana kwa basi la usafiri wa umma na treni, kutokana na ubovu wa miundombinu. Mnamo mwezi Juni 2015, Tunisia ilikumbana na moja ya tukio mbaya zaidi katika historia yake ya hivi majuzi, na vifo vya watu 18 katika ajali kati ya treni na lori huko El Fahes, karibu kilomita sitini kusini mwa Tunis. REUTERS - ZOUBEIR SOUISSI
Matangazo ya kibiashara

"Ajali hii ya treni mbili kugongana imesababisha watu 95 kujeruhiwa, ambao wamesafirishwa hadi hospitali," msemaji wa kikosi cha Ulinzi wa Raia, Moez Treaa ameliambia shirika la habari la AFP, na kuongeza kuwa treni moja ilikuwa imebeba abiria, huku ya pili ikiwa tupu.

Kulingana na msemaji huyo, wengi wa waliojeruhiwa walivunjika mifupa au wamepata majeraha madogo au walikuwa katika hali ya mshtuko, lakini hakuna kesi vifo iliyoripotiwa. Magari 15 ya kubebea wagonjwa na magari mengine ya dharura yametumwa kwenye eneo la ajali.

Ajali ya treni mbili za shirika la reli la Tunisia (SNCFT) imetokea mwendo wa 09:30 saa za Tunisia huko Jbel Jelloud, katika moja ya viunga vya kusini mwa mji mkuu. Sababu za ajali hiyo hazijajulikana.

Mwandishi wa shirika la habari la AFP aliyeshuhudia ajali hiyo anasema aliona sehemu ya mbele anakokaa dereva katika moja ya treni ikiwa imeharibika kiasi. Ajali hiyo ilitokea dakika chache kabla ya kuwasili kwa treni mbili za abiria zilizokuwa zinaelekea kituo kikuu cha Tunis.

Mnamo mwezi Desemba 2016, watu watano walifariki dunia na zaidi ya 50 kujeruhiwa katika eneo moja katika ajali ya kugongana kwa basi la usafiri wa umma na treni, kutokana na ubovu wa miundombinu.

Mnamo mwezi Juni 2015, Tunisia ilikumbana na moja ya tukio mbaya zaidi katika historia yake ya hivi majuzi, na vifo vya watu 18 katika ajali kati ya treni na lori huko El Fahes, karibu kilomita sitini kusini mwa Tunis.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.