Pata taarifa kuu
TUNISIA-USALAMA

Tunisia: Watu wanne wafariki dunia na wengine 7 watoweka baada ya boti yao kuzama

Raia wanne wa Tunisia, akiwemo msichana mdogo, wamefariki na wengine saba hawajulikani walipo baada ya boti iliyokuwa ikibeba wahamiaji kuzama kwenye pwani ya mji mkubwa wa Sfax, katikati-mashariki mwa Tunisia, shirika la habari la AFP limenukuu vyanzo kutoka kwa walinzi wa pwani hiyo siku ya Ijumaa.

Boti mbili za wahamiaji karibu na kisiwa cha Italia cha Lampedusa, Julai 29, 2021.
Boti mbili za wahamiaji karibu na kisiwa cha Italia cha Lampedusa, Julai 29, 2021. AP - Santi Palacios
Matangazo ya kibiashara

"Boti iliyoondoka kutoka pwani ya Tunisia ilizama usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi, karibu na visiwa vya Kerkennah", vilivyoko karibu na Sfax, mji wa pili wa nchi hiyo kwa ukumbwa, msemaji wa kikosi cha ulinzi Houssem Eddine Jebabli ameliambia shirika la habari la AFP.

"Kulingana na shuhuda mmoja, kulikuwa na wahamiaji 32 ndani ya boti hiyo, wote wakiwa raia wa Tunisia. Tuliokoa  watu 21 na kupata maiti ya kwanza haraka," afisa huyo amesema.

Tangu wakati huo, kulingana na afisa huyo, walinzi wa pwani "wameokoa miili mingine mitatu ikiwa ni pamoja na maiti ya msichana", mwenye umri wa miaka kumi, kulingana na vyombo vya habari katika mji wa Sfax.

"Shughuli za kutafuta watu wengine waliopotea zinaendelea," ameongeza msemaji huyo.

Kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), zaidi ya watu 2,500 walikufa au kutoweka baharini mwaka 2021, wakijaribu kuingia Ulaya, hasa Italia, Uhispania au Ugiriki, kupitia njia ya bahari ya Mediterania na Kaskazini Magharibi mwa Afrika.

Kati ya wahamiaji zaidi ya 115,000 waliowasili Ulaya mwaka jana, zaidi ya 20% walitoka Tunisia, nchi ambayo imekuwa na ukuaji dhaifu kwa miaka 10 na ambapo kiwango cha ukosefu wa ajira hivi karibuni kilizidi 18%, na kiwango ambacho kilifikia karibu 41% vijana wakiwemo wahitimu wa vyuo vikuu.

Nchi hiyo, ambayo ilikuwa chimbuko la maandamano ya umma (Arab Spring) mwaka 2011, imekuwa ikipitia mgogoro mkubwa wa kisiasa tangu mapinduzi ya Rais Kais Saied Julai 25.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.