Pata taarifa kuu
TUNISIA-HAKI

Tunisia: HRW yashutumu watu kuzuiliwa kwa maeneo ya siri chini ya hali ya hatari

Nchini Tunisia, shirika la kimataifa la kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch linashutumu vitendo vya watu kuzuiliwa katika maeneo ya siri chini ya baadhi ya vibali vya kifungo cha nyumbani. Tangu rais wa Tunisia ajipe mamlaka makubwa Julai 25, visa vya watu kuzuiliwa nyumbani vinaripotiwa mara kwa mara.

Rais wa Tunisia Kaïs Saïed, Septemba 20, 2021 akiwa katika mji wa Sidi Bouzid.
Rais wa Tunisia Kaïs Saïed, Septemba 20, 2021 akiwa katika mji wa Sidi Bouzid. AP - Slim Abid
Matangazo ya kibiashara

Human Rights Watch inaorodhesha vigogo wanne wa upinzani wa kisiasa wanaodaiwa kuwa chini ya kifungo cha nyumbani ambao kwa hakika wanazuiliwa katika maeneo ya siri.

"Serikali ya Tunisia haizingatii haya kuwa kizuizini katika maeneo ya  siri," amesema. Inaita kifungo cha nyumbani. Na Waziri wa Mambo ya Ndani, katika taarifa kwa vyombo vya habari, amebaini hivyo. Alisema ni kifungo cha nyumbani kama hatua ya tahadhari iliyoamriwa na hitaji la kulinda usalama wa taifa. Alitaja sheria  kuhusu hali tahadhari, " Ahmed Benchemsi, mkurugenzi wa mawasiliano wa Human Rights Watch katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.

"Ukiukaji huu umeongezeka"

"Lakini sheria yote hii haina maana kwa sababu,  kama mtu anakamatwa na polisi waliovaa kiraia, hawamwambii wanampeleka wapi, hawamwambii anachotuhumiwa, na familia yake haiambiwi sehemu anakozuiliwa, kwa zaidi ya mwezi mmoja, haruhusiwi kupata wanasheria wake. Ukiukwaji huu umeongezeka," anahitimisha Ahmed Benchemsi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.