Pata taarifa kuu
DRC-AMANI

Rais wa DRC aonya raia wake kuhusiana na chuki na ukabila

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi anaonya kuwa ongezeko la matamshi ya chuki na ukabila, ni mambo ambayo yanatishia umoja wa taifa hilo. 

Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi wakati akilihutubia taifa Ijumaa Oktoba 22 2021.
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi wakati akilihutubia taifa Ijumaa Oktoba 22 2021. © Ikulu ya Kinshasa DRC
Matangazo ya kibiashara

Tshisekedi, amewataka wanasiasa, viongozi wa dini na viongozi wa kijadi, kusaidia watu kutoka makabila mbalimbali katika nchi hiyo kubwa yenye utajiri wa madini, kuishi kwa amani na utulivu. 

Akizungumwa na Mawaziri wake katika kikao cha 49, ametoa wito pia kwa viongozi wa mashirika ya kiraia kuhusika pakubwa na kuwaelimisha wananchi wa taifa hilo umuhimu wa kutanguliza mbele maslahi ya nchi hiyo. 

Aidha, Thisekedi amemtaka Waziri wa sheria pamoja na yule wa usalama wa ndani, kuwachukulia hatua kali wale wote wanaotuma ujumbe wa chuki unaolenga kuwagawa wananchi wa DRC kwa misingi ya kikabila. 

Viongozi wa kikabila wametakiwa pia, kuwa na vikao vya pampka na kujadiliana na raia kuhusu umuhimu wa kuishi pamoja na kuwa wazalendo wa taifa lao. 

Wito huu unakuja, wakati huu, êneo la Mashariki linapoendelea kushuhudia utovu wa usalama, kufuatia makundi ya waasi kuwauwa raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.