Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-SIASA

Marekani yaonya kuwachukulia hatua wanaokwamisha utekelezwaji wa mkataba wa amani

Marekani imebaini kuwa, uongozi wa Sudan Kusini, umeshindwa kutekeleza ipasavyo baadhi ya vipengele muhimu vya mkataba wa amani uliotiwa saini mwaka 2018 na sasa inaonya kuwachukulia hatua wanaokwamisha utekelezwaji huo, hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyowasilishwa kwa bunge ma Marekani, lakini haijawekwa wazi.

Salva Kiir na Riek Machar.
Salva Kiir na Riek Machar. REUTERS/Jok Solomun
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya mambo ya nje katika ripoti yake kwa bunge la Congress, ambayo haijatangazwa hadharani, imesema serikali ya umoja wa kitaifa ilikuwa inasuasua katika kutekeleza ahadi muhimu zilizotolewa chini ya makubaliano hayo, na walishindwa kutekeleza masuala muhimu katika wakati.

Ripoti hiyo imesema miaka 10 baada ya uhuru, Sudan Kusini inasalia kuwa taifa dhaifu na linalokabiliwa na utawala dhaifu, usalama tete na usimamizi mbaya wa fedha na ufisadi mkubwa.

Hata hivyo, rais Salva Kiir wiki hii amesema, utekelezwaji huo unakwenda vema.

Sudani Kusini iliyopata uhuru wake mwaka 2011, haijawa thabiti kufuatia mapigano yanayochangiwa na tofauti za kisiasa kati ya rais Kiir na Makamu wake wa Kwanza, Riek Machar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.