Pata taarifa kuu

Sudan na Sudan Kusini zafungua tena mipaka yao

Baada ya kufungwa kwa zaidi ya miaka 10, mpaka kati ya Sudan na Sudan Kusini inatarajiwa kufunguliwa Ijumaa hii, Oktoba 1, baada ya makubaliano yaliyotiwa saini mwezi wa Agosti mwaka huu kati ya serikali hizo mbili. Sherehe ambapo viongozi kutoka nchi hizi mbili watahudhuria pia imepangwa kwa siku ya leo.

Wakazi wa mkoa wa Abiye, chanzo cha mvutano kati ya Sudan na Sudan Kusini, wanavuka Mto Kiir.
Wakazi wa mkoa wa Abiye, chanzo cha mvutano kati ya Sudan na Sudan Kusini, wanavuka Mto Kiir. AFP - ALI NGETHI
Matangazo ya kibiashara

Jumla ya vituo 7 vya kuvuka vinapaswa kufunguliwa kwenye eneo la mpaka huu wa zaidi ya kilomita 2,000, na kuwezesha usafirishaji wa huru wa bidhaa na watu kuvuka mpaka bila wasiwasi.

Mpaka kati ya nchi hizo mbili umlifungwa rasmi tangu mwaka 2011 kufuatia mzozo wa eneo hilo. Wakati huo, Sudan Kusini ilikuwa imepata uhuru wake. Khartoum na Juba wanapigania udhibiti wa maeneo kadhaa ya mpakani yenye utajiri wa mafuta, pamoja na mkoa wa Abiye. Na huwa mara nyingi zikipeleka majeshi yao katika eneo hilo.

Kwa miaka mingi, uhusiano kati ya nchi hizi mbili umeimarika. Mpaka umekuwa imara zaidi, ukiwezesha watu wa eneo hilo kuja na kwenda kununua bidhaa mbalmbali.

Sudan na Sudan Kusini ambazo zimeanguka kiuchumi, pia zimewezesha kuanza tena kwa usafirishaji wa mafuta ya Sudan Kusini kupitia mabomba yanayopita eneo la Sudan.

Leo, kufunguliwa rasmi kwa mpaka ni tukio kubwa, amebaini mchambuzi wa kisiasa Jok Maduk Jok. Inaonyesha kurudi kwa imani kati ya serikali mbili, iliyoanzishwa na kuanguka kwa utawala wa rais wa Sudan Omar al-Bashir. La muhimu zaidi, itafungua tena njia za usafirishaji kati ya nchi hizo mbili na kufufua uchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.