Pata taarifa kuu
SUDAN-USHIRIKIANO

Waziri Mkuu wa Sudan atoa wito kwa ushirikiano

Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok alihitimisha ziara ya siku tatu nchini Sudan Kusini Jumapili, Agosti 22. Huko Juba, alikutana kwa mazungmzo na wenzake wa kusini, rais Salva Kiir na makamu wa rais Riek Machar, kuhusu kuundwa kwa jeshi la umoja.

Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok huko Berlin, Ujerumani, Februari 2020.
Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok huko Berlin, Ujerumani, Februari 2020. REUTERS - HANNIBAL HANSCHKE
Matangazo ya kibiashara

Abdallah Hamdok alisafiri kwenda Juba kama mwakilishi wa IGAD, shirika la ushirikiano wa kikanda na kama waziri mkuu wa Sudan. Abdallah Hamdok amebaini kwamba anahusika katika mchakato wa amani nchini Sudan Kusini.

Amejitokeza kama mpatanishi katika mzozo wa kisiasa unaoendelea kati ya rais Salva Kiir na naibu wake Riek Machar. Khartoum pia imeelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya mapigano yayaliyotokea hivi karibuni katika nchi hiyo, katika jimbo la White Nile, kati ya makundi tofauti ya Machar.

Sudan Kusini inakabiliwa na vurugu zisizokoma kwani usitishaji wa mapigano unakiukwa mara kwa mara na makundi tofauti ambayo yanagawana madaraka huko Juba, licha ya mchakato wa amani  mnamo 2018 ambapo Sudan ni mpatanishi.

Kufunguliwa kwa mipaka na maendeleo ya biashara

Abdallah Hamdok aliwasili kutoka Khartoum na ujumbe mkubwa, pamoja na mawaziri wa Mambo ya nje, Ulinzi, Biashara na Madini na Rasilimali za Mafuta, Abdallah Hamdok pia amekaribisha kuimarika kwa ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.

Suala la kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili pia limejadiliwa. Kuanzia Oktoba 1, vituo vya mipaka 4 vitafunguliwa tena baada ya kufunfwa kwa miaka 11. Nchi hizo mbili zimejitolea kuendeleza biashara kupitia ujenzi wa barabara mpya na ukarabati wa reli inayoziunganisha.

Juba na Khartoum pia wamekubali kuanza tena mazungumzo juu ya mkoa wa Abyei. Chanzo cha mgogoro kati ya nchi hizo mbili tangu uhuru wa Sudan Kusini. Eneo hili lenye rasilimali kubwa ya mafuta linadhibitiwa na Khartoum lakini Juba inadai kuwa ni moja ya mikoa yake.

Kura ya maoni inapaswa kufanyika ncini Sudan Kusini, lakini pande hizo mbili zinajadili ikiwa kabila za Waarabu za kuhamahama zitashiriki katika mashauriano haya au la. Majadiliano yanatarajiwa kuanza tena hivi karibuni, zimebaini nchi hizi mbili, bila tarehe yoyote maalum kutolewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.