Pata taarifa kuu

UNSC yaidhinisha kwa kauli moja kikosi kipya cha kulinda amani Somalia

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura kwa kauli moja Alhamisi Machi 31 kuundwa kwa kikosi kipya cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia, kiitwacho Atmis, kitakachochukua nafasi ya Amisom ya sasa ambayo ina askari na raia 20,000.

Wanajeshi wa Burundi kutoka kikosi cha Amison nchini Somalia.
Wanajeshi wa Burundi kutoka kikosi cha Amison nchini Somalia. ABDI DAKAN / AU-UN IST PHOTO / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Baada ya miezi mingi ya mazungumzo ya kujenga, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio ambalo (...) linaunda upya Amisom. Sasa ni Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (Atmis),” umetangaza Umoja wa Falme za Kiarabu, ambao ni mwenyekiti wa Baraza la Usalama mwezi u wa huMachi. Muda wa Amisom ulikamilika Machi 31 na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alikuwa amependekeza mapema mwezi huu kudumisha hadi Desemba 31 idadi ya sasa ya wanajeshi, polisi na raia 19,626 hasa. Kulingana na azimio lililopigiwa kura siku ya Alhamisi, mpango wa kupunguza wafanyakazi wa Atmis utafanywa kwa awamu nne hadi kuondoka kwa wafanyakazi wote mwishoni mwa mwaka 2024.

Idadi ya wanajeshi kupunguzwa

Zoezi la kwanza la kupunguza askari 2,000 linapaswa kufanyika kufikia Desemba 31, 2022, kisha zoezi hilo litafanyika mara kadhaa mwishoni mwa kila hatua (mwezi Machi 2023, mwezi Septemba 2023, mwezi Juni 2024 na mwezi Desemba 2024), kulingana na nakala ya azimio hilo. Somalia, na hasa mji mkuu wake Mogadishu, imeendelea kukumbwa na mashambulizi mengi katika wiki za hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na mawili yaliyotokea wiki iliyopita katikati mwa nchi, shambulio liliyodaiwa na Al Shabab na ambayo liliua takriban watu 48. Wakati huo huo, nchi hii imesubiri kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa uchaguzi wa bunge jipya na rais mpya. Muhula wa Rais Mohamed Abdullahi Mohamed, anayejulikana kwa jina la Farmajo, ulimalizika mnamo mwezi Februari 2021 bila kuweza kuandaa kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.