Pata taarifa kuu
SOMALIA-USALAMA

Somalia: Zaidi ya Thelathini wauawa katika mashambulizi katikati ya nchi

Mashambulizi kadhaa ya kujitoa mhanga yaliukumba mji wa Beledweyne, kaskazini mwa Mogadishu, Jumatano jioni Machi 23, 2022. Watu kadhaa waliuawa katika mashambulizi haya, kwa mara nyingine yakidaiwa na kundi la wanajihadi la Al Shabab, ambalo awali lilifanya shambulio dhidi ya "eneo la kijani" la mji mkuu ambapo uwanja wa ndege unapatikana. 

Mwili wa Mbunge Amina Mohamed Abdi na mhanga mwingine wa shambulio la Machi 23, 2022 huko Beledweyne, kaskazini mwa Mogadishu, Somalia.
Mwili wa Mbunge Amina Mohamed Abdi na mhanga mwingine wa shambulio la Machi 23, 2022 huko Beledweyne, kaskazini mwa Mogadishu, Somalia. AFP - HASSAN ALI ELMI
Matangazo ya kibiashara

Jioni, moja ya mashambulizi haya yalilenga mtu muhimu, ambaye ni mwanamke, mmoja wa viongozi wakuu wa upinzani dhidi ya rais anayemaliza muda wake na katika vita dhidi ya tabia ya kutoadhibu uhalifu.

Mwanamke huyo anayejulikana kwa jina la Amina Mohamed Abdi, alikuwa na umri wa miaka arobaini. Alikuwa mbunge anayemaliza muda wake katika Bunge la Somalia na alikuwa akifanya kampeni za kuchaguliwa tena katika baraza la wawakilishi lenye wajibu wa kumchagua mrithi wa Rais Mohamed Abdullahi Mohamed anayejulikana kwa jina maarufu la Farmajo. Amina Mohamed Abdi alikuwa akimshutumu Rais Mohamed Abdullahi Mohamed kwa kuagiza mauaji ya afisa wa ujasusi, Ikran Tahlil, mwaka jana, katika mazingira ambayo wengi walishuku kuwa aliuawa na maafisa wenzake katika idara hiyo.

Siku ya Jumatano jioni, bomu lililipuka alipokuwa akitoka nje ya makazi ya gavana, na kumuua papo hapo, pamoja na mbunge mwengine na waziri wa zamani. Shambulizi la pili liliukumba mji huo muda mchache baadaye, na lilenga hospitali ambayo wahanga walikuwa wamepelekwa.

Waziri Mkuu wa Somalia alielezea huzuni wake akisema "jukumu la Amina katika kutafuta haki kwa marehemu Ikran Tahlil linajulikana" . "Aliuawa ili haki isitendeke," aliongeza.

Mauaji yake pia yalilaaniwa na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na watu kadhaa wa kigeni ambao walijua kazi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.