Pata taarifa kuu
CAR-MAZUNGUMZO

CAR: Vyama vyote vya upinzani vyatangaza kususia mazungumzo ya kitaifa

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, mazungumzo ya kitaifa yanaanza Jumatatu hii, Machi 21, 2022. Mazungumzo haya yaliyoahidiwa tangu mwaka mmoja na nusu uliyopita na Rais Touadéra, yanatarajia kukomesha mgogoro huo unaoikumba nchi hiyo.

Askari wa jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati karibu na Manispaa ya Jiji huko Bambari, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Novemba 16, 2020.
Askari wa jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati karibu na Manispaa ya Jiji huko Bambari, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Novemba 16, 2020. AFP - CAMILLE LAFFONT
Matangazo ya kibiashara

Dakika za mwisho vyama vyote vya upinzani vilivyoshiriki katika maandalizi hayo hadi sasa vimetangaza kwamba vinasusia mkutano huo kwa madai kuwa madai yao hayajatekelezwa.

Upinzani ulitaka hasa kujumuishwa kwa makundi yenye silaha na mzozo wa uchaguzi wa 2020 kushughulikiwa.

Mkuu wa Umoja wa Mataifa apinga unyanyasaji unaofanywa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Katika ripoti yake ya mwezi Februari mwaka huu iliyowasilishwa mbele ya Baraza la Usalama, Antonio Guterres alivinyooshea kidole cha lawama vikosi vya usalama na jeshi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, pamoja na "washirika wao wa kigeni", akiwataja kwa neno hili mamluki wa kundi la Wagner.

Katika ripoti yake, mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alikaribisha usitishaji vita uliotangazwa tarehe 15 Oktoba na Rais Touadéra lakini alisikitishwa na kukosekana kwa maendeleo yanayoonekana tangu wakati huo. Kwa upande mmoja, mvutano wa kisiasa unaendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, mazungumzo ya kitaifa yamesimama, na hivyo kuweka ugumu makubaliano ya mwaka 2019.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.