Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

Emmanuel Macron na Macky Sall watafakari juu ya misaada ya maendeleo barani Afrika

Jumatano hii, Februari 16, Emmanuel Macron atakuwa pamoja na mwenzake wa Senegal Macky Sall, rais wa sasa wa Umoja wa Afrika. Watashiriki pamoja, mjini Paris, katika hafla ya Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).

Macky Sall na Emmanuel Macron, katika Ikulu ya Γ‰lysΓ©e, Mei 17, 2021.
Macky Sall na Emmanuel Macron, katika Ikulu ya Γ‰lysΓ©e, Mei 17, 2021. Β© Pierre RenΓ©-Worms/RFI
Matangazo ya kibiashara

Tukio hili, mfano wa mkutano kuhusu "jinsi ya kuwekeza" kwa "muungano mpya kati ya Afrika na Ulaya", ni sehemu ya kutafakari juu ya masuala yanayohusiana na misaada ya maendeleo. Kwa upande wa Ikulu ya Γ‰lysΓ©e, wanazungumza kuhusu "kuanzisha upya kwa programu" hiyo, ni kusema kukagua uhusiano na bara la Afrika katika "masharti, mbinu na malengo", kulingana na duru za kuaminika.

"Hatutaki zawadi"

Marekebisho ambayo yanahusisha hasa semantiki. Wakati wa mkutano wa kilele wa Montpellier, rais wa Ufaransa alipingwa juu ya neno na dhana ya "maendeleo" alilotamka, "hatutaki zawadi" viongozi kutoka Afrika wameendelea kulirejelea.

Hotuba ya Marais Emmanuel Macron na Macky Sall inatarajiwa leo jioni, saa chache kabla ya chakula cha jioni kinachosubiriwa kwa hamu katika Ikulu ya Γ‰lysΓ©e kuhusu mustakabali wa ushiriki wa kijeshi wa Ufaransa na siku moja kabla ya mkutano wa kilele wa Ulaya kati ya Umoja wa Ulaya (EU) na Umoja wa Afrika (AU).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.