Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

Mkutano wa 28 wa Afrika na Ufaransa: Matumaini na matarajio ya vijana walioalikwa

Ufaransa leo Ijumaa, inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa nchi hiyo na mataifa ya bara la Afrika, unaolenga kuimarisha mahusiano kati ya Paris na Afrika. Mkutano ambao karibu vijana 3,000 wa Kiafrika kutoka Afrika na nje ya bara hili wamealikwa. 

Rais Macron amewaalika mamia ya vijana wanaojihusisha na biashara, michezo na wasanii.
Rais Macron amewaalika mamia ya vijana wanaojihusisha na biashara, michezo na wasanii. © RFI/Paulina Zidi
Matangazo ya kibiashara

Rais Emmanuel Macron anatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano huu ambao utafanyika katika mji wa Kusini wa Montpellier, lakini hautahudhuriwa na viongozi wa mataifa ya Afrika.

Badala yake, rais Macron amewaalika mamia ya vijana wanaojihusisha na biashara, michezo na wasanii.

Wiki hii afisa kutoka Ikulu ya rais jijini Paris ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema kuwa rais Macron atatumia mkutano huo kuwasikiliza vijana kutoka barani Afrika na kufahamu fursa na changamoto zinazowakabili katika masuala ya kiuchumi, tamaduni na siasa.

Tangu mwaka 1973, Ufaransa imekuwa ikifanya mikutano kama hii na viongozi wa Afrika kujadili masuala mbalimbali lakini mwaka 2017 rais Macron akizungumza jijini Ouagadougou nchini Burkina Faso alihidi kuwa nchi yake itachukua mfumo mpya wa kushirikiana na mataifa ya Afrika na haitoyaambia mataifa ya Afrika nini cha kufanya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.