Pata taarifa kuu
CHINA-USHIRIKIANO

Waziri wa Mambo ya Nje wa China ziarani Afrika Mashariki

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi anaanza ziara ya siku nne barani Afrika siku ya Jumanne. Atazuru Eritrea, Kenya, na Comoro.

Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China, anaanza ziara ya siku nne katika ukanda wa Afrika Mashariki Jumanne, Januari 4, 2022.
Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China, anaanza ziara ya siku nne katika ukanda wa Afrika Mashariki Jumanne, Januari 4, 2022. ANGELOS TZORTZINIS AFP
Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya pili kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China kuzuru bara hilo katika muda wa mwezi mmoja tu baada ya mkutano wa kilele wa FOCAC (China na Afrika) mjini Dakar. Ziara ambapo itakuwa swali la ushirikiano wa kiuchumi, chanjo dhidi ya Covid-19, lakini pia maswali ya usalama. Madhumuni ya Beijing: kuimarisha uhusiano wake na Afrika Mashariki katika mazingira duni ya usalama.

Kuzorota kwa hali ya usalama katika Pembe ya Afrika inatia wasiwasi Beijing, na ziara hii ya kwanza ya mwaka ya kidiplomasia ya China, ambayo kwa zaidi ya miongo mitatu sasa inaanza ziara zake barani Afrika, kunawatia mashaka viongozi wa China kwa utulivu katika sehemu hii ya dunia ambapo China ina maslahi makubwa, ikiwa na miradi mikubwa ya miundombinu kama vile njia ya Mombasa - Malaba nchini Kenya, lakini pia barabara kuu, mitambo ya kuzalisha umeme na kandarasi zingine zilizotiwa saini kama sehemu ya mradi wa Barabara Mpya za Hariri.

Baadhi pia wanaona kama ishara ya msisitizo kwenye diplomasia ya baharini, Bahari ya Hindi bila shaka na, kwa upande wa Eritrea, kuimarisha usalama kwa minajili ya upatikanaji wa Bahari ya Shamu. Wasiwasi ambao tayari umeonyeshwa wakati wa ujenzi wa kambi ya kwanza ya jeshi la China huko Djibouti mnamo mwaka 2017.

Ikiwa washauri kutoka Jeshi la Ukombozi la Watu wapo barani Afrika, inapotokea mzozo "njia ya China" ya kuwaondoa wafanyakazi wa kampuni zetu "inatokana na mazungumzo na washirika wetu wa Afrika (...)", bado hatuna uzoefu katika masuala ya usalama, amesema Wu Peng kabla ya ziara hii. "Sisi tuko upande wa kifedha," ameongeza mkurugenzi mkuu wa idara ya Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China, "ikiwa raia hawana kazi, makundi ya kigaidi yana yanapata urahisi zaidi wa kusajili wapiganaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.