Pata taarifa kuu

Vikwazo vya Marekani: China yataka kushughulikia uovu kuanzia kwenye mizizi

Beijing inapinga vikwazo vya Washington dhidi ya makampuni ya China yanayotuhumiwa kuchangia usafirishaji wa madawa ya kulevya ya aina ya Fentanyl katika soko la Marekani. Aiana hii ya madawa ya kulevya husababisha makumi ya maelfu ya vifo vya kupita kiasi kila mwaka nchini Marekani.

Picha ya kielelezo kutoka Ofisi ya Mwanasheria huko Utah, Marekani. Imewasilishwa kama ushahidi wakati wa kesi, inaonyesha tembe bandia za oxycodone zilizo na fentanyl zilizokusanywa wakati wa uchunguzi.
Picha ya kielelezo kutoka Ofisi ya Mwanasheria huko Utah, Marekani. Imewasilishwa kama ushahidi wakati wa kesi, inaonyesha tembe bandia za oxycodone zilizo na fentanyl zilizokusanywa wakati wa uchunguzi. AP - Uncredited
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa maafisa wa Marekani wa kupambana na madawa ya kulevya, wanasema vita vilivyo kinyume vinaendeshwa na mashirika haya kutoka China , yanayoshutumiwa kushiriki katika uzalishaji haramu wa Fentanyl kwa soko la Marekani.

Kampuni nne na fanyabiashara mmoja wa madawa ya kulevya wanalengwa na vikwazo hivi nchini China; ujumbe ulio thabiti, kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani, ulioelekezwa kwa mashirika ya uhalifu lakini ambao unashangaza utawala wa Kikomunisti.

Hata hivyo ujumbe huo sio mpya. Miaka mitatu iliyopita, wakati wa mapatano ya kibiashara yaliyotiwa saini baada ya mkutano wa G20, China iliahidi kudhibiti vyema uzalishaji wa aina hii ya madawa ya kulevya inayozingatiwa kuwa moja ya sababu kuu za matumizi ya kupita kiasi nchini Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.