Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-HAKI

Afrika Kusini: Baada ya jkisa cha moto, mtuhumiwa afikishwa mahakamani

Moto huo sasa umezimwa katika jengo la Bunge la Afrika Kusini. Moto huo ulizuka tena Jumatatu mchana, na kusababisha uharibifu zaidi, kisha kudhibitiwa usiku.

Zandile Christmas Mafe alifikishwa mbele ya mahakama ya Afrika Kusini Jumanne hii, Januari 4, 2022. NI mshukiwa pekee aliye kizuizini kwa tuhuma za moto uliozuka Bungeni.
Zandile Christmas Mafe alifikishwa mbele ya mahakama ya Afrika Kusini Jumanne hii, Januari 4, 2022. NI mshukiwa pekee aliye kizuizini kwa tuhuma za moto uliozuka Bungeni. REUTERS - SUMAYA HISHAM
Matangazo ya kibiashara

Jengo la Bunge liliharibiwa kama vile Chumba cha zamani, jengo la asili lililojengwa mwisho wa karne ya 19. Hijajulikana sababu ya tukio hilo, lakini mshukiwa mmoja pekee amefikishwa mahakamani Jumanne, Januari 4, 2022.

Wizi, uchomaji moto na kuweka kifaa cha kulipuka ni mashtaka yanayomkabili Zandile Christmas Mafe. Mtu huyu mwenye umri wa miaka 49, anayeishi katika kitongoji cha Khayelitsha, alikamatwa wakati wa moto ulipozuka katika jengo la Bunge.

Inasemekana aliingia ndani ya majengo ya Bunge kupitia dirisha la ofisi. Kamera za usalama (CCTV) zilimnasa mwendo wa saa 2 asubuhi, lakini hakuna mlinzi aliyewekwa nyuma ya mitambo ya kamera hizo ili kutoa tahadhari.

Mtu huyo hakueleza sababu ya kuwepo kwake katika eneo la tukio wakati aliposikilizwa kwa mara ya kwanza mahakamani, lakini alikana mashitaka. Akiwa amevalia shati la kijivu, mshukiwa alionekana kupotea katikati ya kamera zilizomzunguka.

Zandile Christmas Mafe atasalia gerezani hadi Jumanne ya wiki ijayo, tarehe ya kusikilizwa tena. Imeahirishwa hadi wiki ijayo ili kuweza kufanya uchunguzi kamili. Kuzuka tena kwa moto huo Jumatatu alasiri kuliwazuia wataalam kwenda kwenye kile walichoeleza kama "eneo la uhalifu". Wakati huo huo, upinzani unaituhumu serikali kwa uzembe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.