Pata taarifa kuu
LIBYA-UCHAGUZI

Hofu yatanda Libya siku mbili kabla ya tarehe iliyopangwa kufanyika uchaguzi

Baada ya siku kadhaa za mashakana mivutano, mamlaka nchini Libya imebaini leo Jumatano kwamba uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Ijumaa hautafanyika, huku Tume ya Uchaguzi ikipendekeza kuahirisha kwa mwezi mmoja tarehe hii muhimu ya mchakato wa mpito unaopaswa kuiondoa nchi hii katika uhasama wa baadaya Gaddafi.

Zoezi la kupiga kura huko Benghazi, mashariki mwa Libya, Juni 25, 2014.
Zoezi la kupiga kura huko Benghazi, mashariki mwa Libya, Juni 25, 2014. REUTERS/Esam Omran Al-Fetori
Matangazo ya kibiashara

Wataalam wanaona kwamba hali hii inathibitisha kupandwa kwa joto la kisiasa ambalo linaweza kusababisha nchi hii inatumbukia katika"mgogoro mrefu juu ya tarehe ya uchaguzi mpya."

Chini ya saa 48 kabla ya siku hiyo ya uchaguzi, kamati ya bunge inayohusika na ufuatiliaji wa kura imehitimisha kuwa "haiwezekani" kufanyika kwa uchaguzi kwa tarehe iliyopangwa, ambayo ilikuwa imetangazwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Hitimisho lake liliwekwa hadharani baada ya tangazo la kuahirishwa kwa uchaguzi likisubiriwa kwa siku kadhaa, kutokana na kutokubaliana kati ya kambi pinzani.

Tangu kuangushwa kwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011, Libya imeshindwa kujinasua kutoka katika mwongo mmoja wa machafuko, yaliyoshuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni na kuwepo kwa serikali hasimu Mashariki na Magharibi mwa nchi hiyo na mfululizo wa migogoro ya silaha. Uchaguzi wa Desemba 24 ulikuwa wa kuashiria kilele cha mchakato wa kisiasa unaofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kumaliza sura hii ya migawanyiko na ukosefu wa utulivu.

Lakini "baada ya kuona ripoti za kiufundi, kisheria na kiusalama, tunawafahamisha kwamba haitowezekana uchaguzi kufanyika Desemba 24, 2021 kama ilivyoainishwa na sheria ya uchaguzi", ameandika mwenyekiti wa tume hiyo, Al-Hadi al-Sghayer, katika ripoti kwa spika wa bunge, bila kutangaza tarehe mpya ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.