Pata taarifa kuu
LIBYA-SIASA

Mamlaka ya Libya yakataa mtoto wa Gaddafi kuwania katika uchaguzi

Libya haitatawaliwa na Gaddafi mpya: miaka kumi na moja baada ya uasi uliomng'oa madarakani Muammar Gaddafi, mamlaka ya uchaguzi nchini humo siku ya Jumatano ilikataa kugombea kwa mtoto wake mdogo Seif al-Islam katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Desemba 24.

Seif al-Islam (kulia), 49, aliwasilisha faili zake kwa Sebha (kusini), mojawapo ya vituo vitatu vya kuwasilisha maombi ya kuwania katika uchaguzi wa urais, pamoja na Tripoli (magharibi) na Benghazi (mashariki).
Seif al-Islam (kulia), 49, aliwasilisha faili zake kwa Sebha (kusini), mojawapo ya vituo vitatu vya kuwasilisha maombi ya kuwania katika uchaguzi wa urais, pamoja na Tripoli (magharibi) na Benghazi (mashariki). STRINGER libyan High National Electoral Comission FB Page/AFP
Matangazo ya kibiashara

Seif al-Islam Kadhafi anayetafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa "uhalifu dhidi ya binadamu", ambaye aliwasilisha ombi lake Novemba 14, ni miongoni mwa wagombea 25 ambao faili zao zilikataliwa, kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Baraza Kuu la Uchaguzi (HNEC).

HNEC ilieleza kuwa imekataa maombi hayo kwa misingi ya nakala kadhaa za kisheria pamoja na barua ilizopokea kutoka kwa mwendesha mashtaka mkuu wa jamhuri, mkuu wa kikosi cha polisi wa jinai na ukaguzi mkuu wa mamlaka ya uhamiaji.

“Majina yaliyotajwa yametolewa kwenye orodha ya awali ya wagombea kwa sababu hayakidhi masharti yanayotakiwa na hawajaweka nyaraka zote muhimu kwenye mafaili yao,” HNEC imesema.

kwa kutetea hatua ya Seif al-Islam Gaddafi kukataliwa kuwania katika uchaguzi wa urais, HNEC imetumia hasa ibara za sheria ya uchaguzi zinazoeleza kwamba mgombea yeyote "hapaswi kuhukumiwa kwa uhalifu usio na heshima", na lazima awasilishe hati zake kutoka polisi ya jinai inayoonesha kuwa hana hata yoyote waka kutofuatiliwa na mahakama.

Alitekwa Novemba 2011 na kundi lenye silaha huko Zenten kaskazini-magharibi mwa Libya, alihukumiwa kifo mwaka 2015 baada ya kesi ya haraka.

Utawala wa zamani

Kundi hilo hilo dogo hata hivyo lilikataa kumfikisha kwa mamlaka au kwa ICC, ambayo imekuwa ikimsaka tangu 2011 kwa "uhalifu dhidi ya binadamu".

Kundi hilo lilimwachilia mnamo mwaka 2017.

Kwa mshangao mkubwa, Seif al-Islam, 49, aliwasilisha faili zake kwa Sebha (kusini), mojawapo ya vituo vitatu vya kuwasilisha maombi ya kuwania katika uchaguzi wa urais, pamoja na Tripoli (magharibi) na Benghazi (mashariki).

Siku iliyofuata, vigogo kutoka miji kadhaa walitoa wito wa kususia uchaguzi wa urais na vituo kadhaa vya kupigia kura vilifungwa magharibi mwa nchi kwa shinikizo la makundi yanayopinga kuwania kwa Seif al-Islam.

Kilele cha mchakato mgumu unaofadhiliwa na Umoja wa Mataifa, uchaguzi wa urais wa Disemba 24 na uchaguzi wa wabunge uliopangwa kufanyika mwezi mmoja baadaye unadaiwa kugeuza ukurasa katika muongo mmoja wa machafuko na mapambano ya kindugu tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi aliyeuawa mwaka 2011 wakati wa mapinduzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.