Pata taarifa kuu
LIBYA-SIASA

Seif Al Islam, mtoto wa Gaddafi, kuwania kiti cha urais Libya

Hatimaye mahakama nchini Libya imeidhinisha uamuzi wa kumruhusu mtoto wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Moammar Ghaddafi, Seif Al Islam Gaddafi, kushiriki katika kinyang’anyiro cha urais. Mahakama hiyo imepindua umuzi wa tume ya taifa ya uchaguzi (HNEC) wa kumuondoa kwenye orodha ya wagombea urais kwa madai ya kutokidhi vigezo.

Seif al-Islam Kadhafi, ambaye anasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa tuhuma za uhalifu wa kivita, ameidhinishwa na mahakama ya mkoa wa Kusini wa Sabh,kushiriki katika kinyang'anyiro cha urais Libya.
Seif al-Islam Kadhafi, ambaye anasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa tuhuma za uhalifu wa kivita, ameidhinishwa na mahakama ya mkoa wa Kusini wa Sabh,kushiriki katika kinyang'anyiro cha urais Libya. Mahmud TURKIA, - AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Seif al-Islam Kadhafi anayetafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa "uhalifu dhidi ya binadamu", ambaye aliwasilisha ombi lake Novemba 14, ni miongoni mwa wagombea 25 ambao faili zao zilikataliwa, kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Baraza Kuu la Uchaguzi (HNEC).

HNEC ilieleza kuwa imekataa maombi hayo kwa misingi ya nakala kadhaa za kisheria pamoja na barua ilizopokea kutoka kwa mwendesha mashtaka mkuu wa jamhuri, mkuu wa kikosi cha polisi wa jinai na ukaguzi mkuu wa mamlaka ya uhamiaji.

Hatua hiyo ya mahakama ya mkoa wa Kusini wa Sabha, ilitangazwa jana Alhamisi baada ya Seif al-Islam kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa wiki iliyopita wa tume kuu ya uchaguzi nchini Libya, kumuondoa katika orodha ya wagombea kwa kumtuhumu makosa ya zamani yanayohusiana na kutumia mabavu dhidi ya waandamanaji.

Hatua hii ya mahakama inampa nafasi kugombea urais katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika tarehe 24 mwezi huu wa Desemba.

Katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Al Islam aliwashukuru majaji kwa kuhatarisha usalama wao akisema wamefanya hivyo ''kusimamia ukweli.'' Pia aliishukuru familia yake na wafuasi wake.

Uchaguzi huo unakuja baada ya miaka mingi ya majaribio yanayoongozwa na Umoja wa Mataifa kutafuta mustakabali wa kidemokrasia na zaidi sana kumaliza vita vya wenyewe nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.