Pata taarifa kuu
MISRI-HAKI

Misri: Mtetezi wa haki za binadamu Patrick Zaki aachiliwa huru baada ya miezi 22 jela

Baada ya miezi 22 kizuizini nchini Misri, Patrick Zaki, mtafiti wa Misri kuhusu suala la jinsia na mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Bologna nchini Italia, ameachiliwa Jumanne, Desemba 7. Kesi ya mwanaharakati wa haki za binadamu wa kanisa la Coptic kuhusu makala inayokemea ubaguzi dhidi ya Wakristo nchini Misri itaendelea tena Februari 1, 2022.

Huko Bologna, bango la kumuunga mkono Patrick Zaki.
Huko Bologna, bango la kumuunga mkono Patrick Zaki. AP - Gregorio Borgia
Matangazo ya kibiashara

Patrick Zaki, mtafiti wa Misri mwenye umri wa miaka 27, alikamatwa Februari 2020. Nakala ya kiini cha kesi hiyo ilichapishwa mwaka 2019 kwenye tovuti ya habari ya Daraj. Alisimulia maisha ya kila siku ya Wakristo wachache wa kanisa la Coptic huko Misri kama shajara.

Patrick Zaki, aliyesomea Bologna, Italia, pia alifanya kazi katika Taasisi ya Misri ya Haki za Kibinafsi (EIPR). Katikati ya mwezi Septemba, shirika moja la haki za binadamu lilishutumu Cairo kwa kuvunja kupitia kesi hii uhuru wa kujieleza "wa Wamisri wote" na "haki ya Wakristo wa Misri kudai (...) 'usawa'.

Nchini Italia, hatima ya Patrick Zaki ilifuatwa kwa karibu. Ombi lilikuwa limekusanya maelfu ya saini za kuachiliwa kwake. Mnamo Aprili Bunge la Seneti pia lilipiga kura ya kumpa uraia wa Italia. Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Luigi Di Maio, pia ametangaza haraka kwenye Twitter baada ya tangazo la kuachiliwa kwake, "lengo la kwanza limefikiwa: Patrick Zaki hayuko tena gerezani".

Patrick Zaki anakabiliwa na kifungo cha miaka 5 jela kwa "habari za uwongo". Kesi hiyo inayoendeshwa katika mahakama ya kipekee, mahakama ya dharura ya Usalama wa Jimbo la Mansoura, Patrick Zaki hataweza kukata rufaa.

Misri ina zaidi ya wafungwa 60,000 wa maoni, kulingana na mashirika yasio ya kiserikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.